Noma Sana .. Steve Nyerere Afunguka ya Moyoni Baada ya Nape Kutumbuliwa,Amtaka Afanye Hivi..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Muigizaji maarufu wa vichekesho  Steve Nyerere amemshauri Mh.Nape Nauye kumshukuru Mungu na kumuomba kwa kutenguliwa uwaziri kwa kuwa hajui ameepushwa na jambo gani.

Akiongea na eNewz Steve Nyerere ameendelea kusema kwamba Mh. Nape nje ya uwaziri alikuwa ni msanii pia na alikuwa anaithamini thamani ya msanii na kuilinda pia alikuwa akipenda maendeleo ya wasanii na maendeleo yake na alikuwa na uwezo wa kupiga simu hata usiku kufuatilia masuala ya sanaa.

Amemshauri Nape aendelee kuwa karibu na wasanii na kuwashauri kwa ajili ya kusukuma mbele maendeleo ya sanaa nchini.

"Nape kama waziri aliyekuwepo, ajue kuwa ana jukumu la kuwashauri wasanii kupiga hatua, kuondoka kwake siyo kuwakimbia wasanii, abaki kuwa mshauri wa wasanii kupiga hatua na kusonga mbele.. Nape ana uwezo mkubwa sana, ana ushawishi mkubwa sana" Amesema Steve

Hata hivyo Steve alimalizia kwa kumshauri Nape kukaa na familia yake na kusali kwa kuwa Mungu ndiye alipanga apewe madaraka ya kuwasimamia wasanii lakini pia amshukuru kwa kuchukua cheo hicho kwa kuwa hajui Mungu kamuepusha na nini na asiogopeshwe na miguno ya wananchi"

Steve pia amemsihi Dkt. Mwakyembe kukabiliana na changamoto lukuki zinazoikabili sanaa
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad