Fahamu Kwanini Matajiri Huendelea Kuwa Matajiri na Masikini Huendelea Kuwa Masikini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Leo nimeona nilete elimu fupi juu ya makundi haya matatu ya watu waishio hapa ulimwenguni, ambao ni MATAJIRI (The rich), WATU WA MAISHA YA KATI (The middle class) na MASIKINI (The poor).

1.MATAJIRI
Nikianza na kundi hili, tafsiri halisi ya neno au kundi la watu hawa ni tofauti sana na mtazamo wa waliowengi. matajiri ni wale watu ambao humiliki Biashara kubwa au wamewekeza (invest) katika biashara kubwa na ambapo hupata pesa ikiwa wapo au hawapo eneo husika. Pia kwa tafsiri nyingine ni watu ambao pesa yao huwafanyia kazi au kuwaajiri watu wengine wawafanyie kazi. mfano; Bill gates, Aliko dangote, Mo dewji n.k (wawekezaji na wamiliki wa biashara kubwa)

2.WATU WA KIPATO CHA KATI
Hili ni kundi ambalo watu wengi hudhani kuwa ni matajiri lakini si kweli na hii yote ni kutokana na mwenendo na hali ya maisha ya watu hawa. Hapa nawazungumzia wale watu walio ajiriwa na kupokea mishahara minono, wamiliki wa biashara ndogo, na wale wenye taaaluma(specialists or talents) mbalimbali au kwa lugha nyepesi ni wale watu wanaotumia Muda, Nguvu na Akili zao kupata kipato yaani kama ikitokea mtu huyu hayupo eneo husika basi ndio unakuwa ukomo wa kupata kipato. mfano, wanamichezo, waajiriwa.

3.MASIKINI
Hapa tunawakuta wale wote ambao hushindwa kutimiza mahitaji muhimu katika maisha yao ikiwamo kula, kulala na hata mavazi yaani BASIC NEEDS kwa lugha ya kiingereza. Na maisha ya kundi hili mara yingi yamekuwa ni ya kukumbwa na simanzi, huzuni na kushindwa kupiga hatua kimaendeleo kutokana na sababu kadha wa kadha.


Vilevile ningependenda kugusia swali fupi ''Kwanini Matajiri wanazidi kuwa matajiri, Masikini wanazidi kuwa masikini na watu wa maisha ya kati wanabaki hapohapo walipo siku zote?''

''why the rich get richer, the poor get poorer and the middle class are getting squezed out?''

Siri kubwa hapa si kitu gani watu hawa hufanya bali ni kitu/vitu gani watu hawa hununua. 

Nikianza na MATAJIRI kundi hili mara zote wamekuwa ni watu wa kununua vitegauchumi (assets) na ninaposema assets ama vitegauchumi simaanishi nyumba ya kuishi, magari au vitu vingine vya thamani bali ni vile vyote ambavyo ukinunua vinauwezo wa kukulipa (something that pays you money). Mfano nyumba kwa ajili ya biashara (real estate), gari kwa ajili ya biashara, Hisa (stocks), bond n.k

WATU WA MAISHA YA KATI (middle class) watu hawa hununua madeni yaani (LIABILITIES) ninaposema madeni ni kwamba watu hawa hununua vitu ambavyo hutoa pesa mifukoni mwao (somethings that cost money) mfano. gari la kutembelea, nyumba ya thamani ya kuishi, tena vile vile wengine hata hudiriki kuchukua mikopo bank ili wafanikishe hayo.

MASIKINI hawa siku zote hununua vitu ambavyo havina umuhimu sana maishani mwao.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad