HAJI Manara - Kama Mbwai na Iwe Tu..Niko Tayari kwa Mapambano na TFF ya Malinzi..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mkuu wa  Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Haji Manara amesikitishwa na uamuzi uliotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) huku akidai yupo tayari kwa mapambano kwa kuwa hakupewa nafasi ya kusikilizwa. 

Haji Manara amesema hayo baada ya kutolewa  hukumu na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu, Jerome Msemwa ya kumfungia kujihusisha na masuala ya soka kutokana na makosa matatu ambayo ni kuituhumu na kuidhalilisha TFF, kueneza chuki za ukabila kwa kudai Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu wake Selestine Mwesigwa kuwa ni Wahaya na viongozi wa zamani wa Yanga na la mwisho kuingilia utendaji wa shirikisho hilo.

Kufuatia maamuzi hayo ya TFF Manara amefunguka haya 

"Unazuia na kutonipa nafasi ya kusikilizwa, unanipa hukumu kwa makosa nisiondikiwa katika mashtaka yao..Nipo tayari kwa ajili ya mapambano, tukutane juu". Alisema Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram

Haji Manara amesimamishwa kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja na pia kutakiwa kulipa faini ya Shilingi Milioni tisa.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kuna makosa mengi ndani ya TFF kwa hili swala,lakini pia Simba watakumbana na rungu kama Haji ataamua kuipeleka juu kisheria kwa maana yataongelewa yote na sababu ya TFF kufikia kumfungia Manara.

    ReplyDelete

Top Post Ad