Ile Kesi ya Kumuua Mvungi Yafikia Hatua Hii..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


WAKAZI sita wa Dar es Salaam wanaotuhumiwa kumuua kwa makusudi aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi, leo wanatarajiwa kusomewa maelezo ya mashahidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya upelelezi wa kesi hiyo kukamilika.

Washitakiwa hao ni John Mayunga (56), Juma Kangungu (29), Longishu  Losingo (29), Paulo Mdonondo (30), Mianda Mlewa (40) na Msungwa Matonya (30).

Maelezo hayo yanatarajiwa kusomwa na Wakili wa Serikali, Patrick Mwita mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wa Mahakama hiyo, ambapo washitakiwa hao waliposomewa mashitaka ya mauaji walikana kuhusika.

Baada ya kusomewa maelezo yao, jalada la kesi hiyo litapelekwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam ili kesi ianze kusikilizwa, kwa sababu Mahakama ya Kisutu kisheria haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Awali, Mwita aliieleza Mahakama kuwa hawawezi kuwasomea maelezo hayo, kwa sababu bado wanashughulikia taratibu za kuliondoa jina la Chibago Magozi kwenye jalada ambalo lipo Mahakama Kuu, kwa sababu bado hawajapata cheti cha kifo licha ya kuandika barua kwa mamlaka husika.

Awali, washitakiwa walikuwa 11 mmoja akafariki dunia na kubaki 10, na kati yao Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Biswalo Mganga aliwasilisha mahakamani nia ya kutoendelea kuwashitaki wanne kwa hiyo wakabaki sita.

Washitakiwa walioachwa huru baada ya kusota rumande kwa miaka minne ni Ahmed Kitabu (30), Zacharia Msese (33), Masunga Makenza (40) na Msungwa.

Inadaiwa kuwa washitakiwa hao Novemba 3, 2013, wakiwa   Msakuzi Kiswegere, Kinondoni, kwa pamoja walimuua Dk Mvungi.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad