Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Makamu wa Rais a chama cha wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Godwin Ngwilimi amekamatwa na polisi huko mkoani Shinyanga na anashikiliwa katika kituo kikuu cha polisi mkoani humo.
Taarifa iliyotolewa na Rais wa TLS Mhe.Tundu Lissu ni kwamba Ngwilimi akiwa katika gari yake alisimamishwa na askari aliyekua kavaa kiraia, akitaka kukagua gari yake.
Ngwilimi alimtaka Askari huyo ajitambulishe kwanza kwa kutoa kitambulisho cha kazi kabla ya upekuzi. Lakini badala ya kujitambulisha alimzuia Ngwilimi na kumuelekeza kituo kikuu cha polisi Shinyanga ambapo anashikiliwa hadi sasa.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA