MGONGANO Huu Bongo Muvi ni Kaburi Jipya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Aprili 19, mwaka huu,  baadhi ya mastaa wa Bongo Muvi, waliandamana kupinga wizi wa  kazi zao na uingizwaji holela wa filamu za nje ambazo huuzwa kwa bei chee hivyo kuua soko la filamu zao.

Hata hivyo, katika mchakato huo, kuliibuka hoja na maswali lukuki kutoka kwa wadau wa filamu hizo, miongoni mwao wakiwemo wasanii wenzao kutoka Bongo Muvi ambao  hawakukubaliana moja kwa moja na mchakato huo. 

Hoja kubwa iliyoibuka ni kwamba siyo uuzwaji holela wa filamu za nje kwa bei chee ndiyo chanzo cha anguko la soko la Bongo Muvi bali ni ubovu wa filamu zao. Mgongano wa kifikra juu ya jambo hili unatajwa kuzidi kupamba moto katika mitandao ya kijami huku hali hiyo ikitafsiriwa kama kaburi jingine jipya la Bongo Muvi kufuatia mpasuko uliopo.

Tafsiri hii inatokana na ukweli kwamba kama wasanii wenyewe wanashindwa kuzungumza lugha inayofanana kubainisha na kutafuta ufumbuzi wa tatizo la anguko lao ni wazi watakuwa wakicheza ngoma isiyokuwa na uelekeo.

Yafauatayo ni baadhi ya maoni ambayo Wikienda limeyapata kutoka kwa baadhi ya wasanii wa Bongo Muvi lililopofanya nao mahojiano kufuatia maandamano hayo.

STEVE NYERERE:

“Wasanii wengi ni waoga, wanashindwa kuzungumza ukweli juu ya nini kinachofanya soko la filamu zetu kudorora, ukweli ni kwamba filamu zetu hazina ubora, tumeishiwa ubunifu ukilinganisha na tulivyoanza, mbona kipindi cha nyuma tulifanya vizuri na filamu za nje zikikuwepo? Tena ziliuzwa kwa bei rahisi kabisa.

Kinachotakiwa ni kuzungumza ukweli kwa viongozi na tuone  nini wanaweza kutusaidia ili tuendane na mahitaji ya Watanzania kwa sasa.”

SIMON  MWAKIFWAMBA: “Mimi bado swali langu kwa hao waliofanya maandamo ni lilelile, je, tupige marufuku kuonesha ligi za mpira wa miguu za nje, kisa ya ligi kuu yetu ya ndani haifanyi vizuri? Jibu  ni hapana.

Kwa hiyo kuna namna ya kujipanga kwa mbinu zingine na siyo haya yanayofanyika.”

DUMA: “Filamu za nje ni vema zikome-shwe kabisa, ukweli ni kwamba hizi ni filamu nzuri na zina mvuto, utengenezaji wao ni wa kiwango cha juu kwa kuwa wenzetu wamewekeza  vya kutosha, tofauti na sisi, hata hivyo filamu hizo zinauzwa kwa bei rahisi kwa wateja wetu.

Unategemea nini zaidi ya kupotea kwa soko letu?
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad