BIBI Kizee wa Miaka 70 Apandishwa Kizimbani Akidaiwa Kuiba Gari..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Fatuma Mohammed (70) na Aziz Njakula (36) wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya wizi na kupatikana na gari la wizi aina ya Toyota Hiace.

Wakili wa Serikali, Hamisi Said amedai  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa Julai 9, 2015 eneo la Mnazi Mmoja walitenda kosa la wizi wa gari hilo mali ya kampuni ya Choice Motors.

Januari 26, 2016 eneo la Nzasa, Dar es Salaam Mohammed anadaiwa alikutwa akiwa na gari la wizi nyumbani kwake.

Baada ya kusomewa mashtaka washtakiwa wamekana na upande wa Jamhuri ulidai upelelezi haujakamilika.

Hakimu Simba ametoa masharti ya dhamana kwamba wawe na wadhamini wawili kila mmoja ambao watasaini bondi ya Sh10 milioni. Walikamilisha masharti na kuachiwa kwa dhamana.

Credit - Mwananchi
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad