GWAJIMA Apanga Kuanika Madudu ya Lipumba Cuf..Maalim Seif Amoa Ubuyu Wote Kuhusu Yaliyotokea..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima amemuweka kiporo Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na kuhoji kwa nini mwenyekiti huyo anaruhusiwa kukivuruga chama hicho.

Askofu Gwajima ameyahoji hayo baada ya kupokea malalamiko ya mgogoro uliopo ndani ya CUF kutoka kwa Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad alipokwenda kumtembelea ofisini kwake, leo Ubungo jijini Dar es Salaam.

“Katika mazungumzo yetu nilitaka kujua Lipumba anafanyaje kuvuruga chama chako ili nami nijue cha kufanya, si unajua tena. Kwa nini unamruhusu kukivuruga chama?” amehoji Gwajima.

Baada ya kuhoji hayo, Gwajima amesema atayatafakari mazungumzo hayo na kwamba baada ya kutafakari atajua cha kufanya sambamba na kuueleza umma kile atakacho kuwa nacho.

“Kwa vile ameniambia mgogoro jinsi ulivyo basi nami najua cha kufanya, na nitakacho kuwa nacho nitasema baadae, ngoja nitafakari kwanza,” amesema.

'Mimi huyu ni rafiki yangu kwa hiyo nilitaka kujua Professa Lipumba anafanya nini kuvuruga CUF, hivyo nilitaka kujua Lipumba amepatwa na nini mpaka amevuruga chama chako na kiukweli mimi nilikuwa siufahamu vizuri huu mgogoro ila saizi Seif ameniambia kwa hiyo na mimi nataka nitafakari alichoniambia rafiki yangu ni 'digest' baada ya hapo nitajua nafanya nini" alisema Gwajima

Nilikuwa siufahamu vizuri mgogoro wa CUF ila sasa Seif ameniambia. Natafakari alichoniambia ni 'digest' halafu nitajua nafanya nini - Gwajima

Kwa upande wake Maalim Seif ambaye alizuru kwa Gwajima kwa ajili ya kumjulia hali na kuzungumza naye masuala mbalimbali ya nchi, amesema anamuunga mkono mchungaji huyo kwa chochote atakacho kufanya.

“Namuunga mkono aliyoyasema, sisi ni marafiki wa muda mrefu nimekuja kumjulia hali na kuzungumza naye mambo mbalimbali na kila mmoja kayaeleza yake,” amesema Maalim Seif.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Gwajima amekuwa 'mchambaji' wa mjini, anakodishwa 'kusutana', hata kama ugomvi haumuhusu na haujui, ukimuelezea anauvaa na kutembeza kichambo.....hahahaha maisha ya mjini raha tupu

    ReplyDelete

Top Post Ad