KAMANDA Sirro - Alichofanyiwa Malima ni Sawa Kabisa na Asillamike kwa Lolote Lile..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro ametoa ufafanuzi kuhusu sakata la askari kufyatua risasi hewani mbele ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima na kusema Polisi walifanya vile ili kuwatia nguvuni watuhumiwa.

Kamanda Sirro amesema hayo  pindi alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari ofisini kwake baada ya kuenea maneno sehemu mbalimbali zikidai polisi hao hawakutumia busara katika kufanya kazi yao.

“Kimsingi ninachosema ile bunduki  tunayowapa askari ni kwaajili ya matumizi na tumewapa maelekezo..Kikubwa wananchi wajue suala la utie wa sheria bila ya shuruti ni la msingi, ukikataa kutii sheria tuna kila namna tunahakikisha tunakukamata na kukupeleka panapo husika. Kwa hiyo askari Polisi alichokifanya ni kutumia uzoefu wake, umakini wake kuhakikisha kwamba gari ambalo ni kielelezo, dereva ambaye ni mtuhumiwa na Mhe. Malima ambaye ni mtuhumiwa wanapelekwa vituo vya polisi na wamefanikisha hicho na leo amepelekwa mahakamani". Alisema Sirro

Katika hatua nyingine, Malima ameachiwa huru kwa dhamana ya Milioni tano baada ya jana kuweka kizuizini na  kupandishwa Mahakamani kwa kosa la kumzuia askari kufanya kazi yake.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad