MAMLAKA ya Hali ya Hewa Nchini Yatahadharisha Mvua Kubwa Zaidi Kuendelea Kunyesha Nchini..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesema wakati msimu wa mvua za masika ukielekea ukingoni, wananchi wanatakiwa kufuatilia taarifa zinazoendelea kutolewa ili kuchukua tahadhari dhidi ya mvua kubwa zinazoweza kutokea.

Msimu wa mvua za masika ulianza Machi na zitamalizika Mei mwaka huu,  katika maeneo ya Ukanda wa Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manaya , Kaskazini, Pwani ya Kaskazini  katika mikoa ya  Morogoro, Pwani, Dar es Salaam, Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba.

Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa wa TMA, Dk. Ladislaus Chang’a, alilieleza Nipashe jana kuwa mvua hizo zimeendelea kupungua wakati zikifikia ukingoni.

“Mvua zinaendelea kupungua, lakini matukio machache ya mvua kubwa yanaweza kuwatokea, hivyo wananchi wanatakiwa kutufuatilia taarifa tunazotoa ili kuchukua tahadhari ingawa zimepungua lakini hatuwezi kusema zimeisha hadi msimu umalizike,” alisema.

Alisema katika maeneo hayo  na yale ya kuzunguka Ziwa Victoria wanapata mvua mara mbili kwa mwaka ambazo ni mvua za vuli na masika na kwamba kwa mwaka huu zilikuwa kubwa.

Alisisitiza kuwa msimu wa mvua bado unaendelea, ingawa zinaelekea ukingoni na kwamba zinaendelea kupungua kabla ya kumalizika kabisa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad