MVUA Yasababisha Maafa Makubwa Mwanza na Bukoba..Yabomoa Barabara Kuu..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mvua imesababisha barabara kuu ya Mwanza -Bukoba kukatika eneo la Kemondo, hivyo magari ya abiria na mizigo kuzunguka Kyetema kupitia Katerero kutokea Muleba.

Barabara hiyo imekatika jana (Ijumaa) saa 11:00 alfajiri kutokana na mvua iliyonyesha usiku kucha na kusababisha maji kujaa kwenye karavati.

Kutokana na hali hiyo wananchi na hasa wafanyabiashara wa eneo la Kemondo wameshindwa kuendelea na shughuli zao kwa kukosa mawasiliano.

Naima Issa, mkazi wa Kemondo amesema wanafunzi wamekatisha masomo baada ya kukosa eneo la kupita.

Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) Mkoa wa Kagera, Andrew Kasamwa amesema watumiaji wa barabara hiyo wanatumia njia mbadala kwa kupita Katerero mzunguko wa umbali wa takriban kilomita 10.

Amesema jitihada zinafanywa kukarabati eneo hilo ili kurejesha mawasiliano.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad