MWIGULU Nchemba: Bado Hatuna Sheria ya Kuthibiti Shisha..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba bungeni  amesema serikali bado haina sheria ya kuthibiti matumizi ya kilevi aina ya shisha ila lipo agizo la Waziri Mkuu la kupiga marufuku biashara hiyo na kutaka agizo hilo lifuatwe na kila mtu.

Mwigulu Nchemba amesema hayo wakati akijibu swali bungeni kuhusu matumizi ya kilevi hicho cha shisha ambacho bado katika baadhi ya maeneo kimeendelea kutumika na kuleta athari kwa watumiaji.

"Ni kweli serikali baada ya kuona matumizi ya kilevi cha Shisha yanaleta athari kwa binadamu, serikali imeanza kuweka sheria za kuthibiti matumizi ya shisha, usambazaji wa shisha na uagizaji wa kilevi hicho, lakini wakati tunasubiri sheria hizo tunatambua kuwa lipo agizo la Waziri Mkuu la kupiga marufuku matumizi ya kilevi cha shisha ambalo utekelezaji wake ulianza mikoani kama Dar es Salaam, Mbeya, Iringa na mikoa mingine imeendelea kuitikia. Kwa hiyo maelekezo ya Mh. Waziri Mkuu yanafanyiwa kazi bila kupunguza hata nukta" alisema Mwigulu Nchemba

Mbali na hilo Waziri Mwigulu alisema anatambua wapo watu walipewa leseni kwa ajili ya kufanya biashara hiyo ya shisha lakini kwa kuwa serikali inajali masuala ya afya ya Watanzania ndiyo maana wanatakakuja na sheria ili kuthibiti kilevi hicho ambacho kina athari kwa watumiaji.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad