Sakata la Mchanga wa Madini… Gwajima: Watanzania Tumerogwa..Nampongeza Rais Magufuli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ulozi! Siku chache tangu liibuke sakata la mchanga wa madini (makanikia), kufuatia ripoti ya kamati maalum iliyoundwa na Rais Dk John Pombe Magufuli kusomwa na kuibua mazito, Askofu wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church (GCTC) ‘Ufufuo na Uzima’, Dk Josephat Gwajima ameibuka na kutema cheche kuwa Watanzania wamerogwa.

Katika mahubiri yake Jumapili ya jana, Askofu Gwajima alimpongeza Rais Magufuli kwa hatua alizochukua na kumtaka azidi ‘kukaza uzi’ kwani Watanzania tunashangaza kuishi kwenye umaskini licha ya nchi yetu kujaliwa rasilimali nyingi ambazo kama zingetumika kwa usahihi tungekuwa tunaogelea kwenye utajiri.

Askofu Gwajima alisema haiwezekani nchi yenye madini mengi zaidi ya 320 anayoyajua, wingi wa mito, maziwa na mbuga za wanyama, lakini bado inaomba msaada ikiwemo wa chakula kutoka kwa mataifa ambayo kwa uhalisia yalitakiwa kuomba msaada kutoka kwetu.

“Nataka niseme ukweli pasipo kupindisha mambo kuwa, sisi Watanzania tumerogwa na mchawi wetu ni special (maalum), kwa sababu haiwezekani kwa nchi yenye utajiri mkubwa kama huu, madini, maziwa, mito, mabonde na mambo mengine yenye kuvutia ikiwemo mbuga za wanyama, lakini bado wananchi wake wanauza karanga na ubuyu, huko ni kurogwa.

“Nampongeza sana Rais Magufuli kwa kuamua kukata utepe ambao ulikuwa umedumu kwa muda mrefu, eti wachimbaji wachukue asilimia zote za madini na kutuachia asilimia nne tu, inaingia akilini kweli? Kuna aina 320 za madini ninayoyajua, mengine hata ukitajiwa majina unabaki unashangaa, sasa watu wanakuja na kuchukua yote, huku sisi tunabaki maskini, sasa kama siyo kurogwa huko ni nini? Watanzania tumerogwa, wewe zaidi ya makontena 277 yalitakiwa yapelekwe nje, hakika tumerogwa na tunatakiwa tuamke sasa,” alisema Askofu Gwajima.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad