WANAUME wa Dar es Salaam Acheni tu Wenzenu wa Mikoani Wawadharau kwa Aibu Kubwa Kama Hii..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Tokea hali hii ya Hewa ya Mvua kubwa na hii baridi ianze kwa takribani kama wiki moja sasa nimekuwa nikipita kwa ' Washikaji ' zangu kuwatembelea lakini nilichokikuta huko Kwao kimesinikitisha mno na kinatia mno aibu.

Huko nyuma nilikuwa ' nachukia ' sana jinsi Wanaume waishio Mikoani walivyokuwa ' wakitudhihaki ' sisi Wanaume wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwa ' lege lege ' huku tuki ' deka deka ' kama Watoto wa Kike kutokana na ' matendo ' yetu lakini kwa aina hii ya ' Upuuzi ' huu nilioushuhudia mwenyewe katika Wanaume kama saba ( 7 ) hivi na bahati nzuri wote hao kila uchao lazima waende ' gym ' kupasha ili ' kujikomaza ' lakini kumbe hamna lolote.

Jamani kwa haka ' kaubaridi ' tu ka uwongo na kweli ni halali kweli Wanaume wa Mkoa wa Dar es Salaam kuoga maji ya moto? Hivi kweli baridi hii iliyopo sasa jijini ni ya kuwafanya Wanaume wa huu Mkoa kusubiri maji yachemke jikoni kisha waweke katika Ndoo zao na wakaoge?

Wanaume wa Mikoani mlikuwa ' mkitudharau ' sisi Wanaume wa huu Mkoa wa Dar es Salaam nami leo naungana nanyi kwa 100% kuwa mnastahili ' kutudharau ' kwani hii ya sisi Kuoga maji ya moto kwa kisingizio cha baridi kali lililopo ni dalili mbaya mno na pengine ndiyo maana hata Wanawake wa Dar es Salaam wanatucheka na kutudhihaki mno.

Wanaume wa Dar es Salaam tubadilikeni upesi na tuoge maji ya baridi tu na tuache kujilegeza na kudekadeka kwa kuoga maji ya moto badala yake hayo maji ya moto tuwaachie Mama na Dada zetu kwani kiukweli ' tunajiaibisha ' mno.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mm ni mwanamke na ni mwiko maji moto yan mm ni maji barid hata iweje na nimeish singida njombe mbea iringa....na huko kote maji nilikua naogea ya barid....lkn hapa utashangaa dume linalia kabisaaa barid...ukiuliza barid ipi eti hii ya dar.. khaa...muache ulege lege mmezid hebu mjikaze maji barid yanachangamsha akili sana....

    ReplyDelete
  2. sio maji ya moto tu,na cream,lotion,rangi za kucha,pamba za masikioni pamba za machoni yaani ni hasara kabisaaaaaaaaaaaa.

    ReplyDelete

Top Post Ad