WATOTO Watatu Waliobaki Katika Ajali ya Gari la Shule ya Luck Vicent ya Arusha Kupelekwa Marekani kwa Matibabu..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Jopo la madaktari bingwa wa Shirika la Stemm la Marekani kwa kushirikiana na Serikali, limeamua kuwapeleka  Marekani kwa matibabu majeruhi watatu  wa ajali ya wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva.

Majeruhi hao ambao wamelazwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru ni Jofrey Tarimo, Doreen Mshana na Sadia Awadh wanatarajiwa kusafirishwa kwenda Marekani wakiambatana na wazazi wao,  daktari na muuguzi wa hospitali ya mkoa wa Arusha.

Matibabu hayo  yatatolewa kwa  ufadhili wa madaktari hao kutoka Marekani ambao walikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuwasidia wanafunzi hao kutoka kwenye gari lililo pata ajali, wakiwa njiani kuelekea Ngorongoro na Serengeti kutalii.

Daktari mkuu wa hospitali Mount Meru,  Wonanji  Thimos  amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na madaktari hao imeshaanza taratibu za kuwasafirisha majeruhi hao kwa ajili ya matibabu zaidi.

Dk Thimos amesema taratibu za safari zikikamilika majeruhi hao watasafirishwa kwenda Marekani wakati wowote kuanzia sasa.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad