EATV na Radio Washutumiwa Kujiendesha Kwa Matakwa ya Watu Wenye Chuki Binafsi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


KUONA OFFICE INAENDESHWA KWA MATAKWA YA WATU WENYE CHUKI BINAFSI NA MTU FLANI NI TATIZO KUBWA.

#CLOUDSMEDIA ni office ambayo ina matatizo yake na baadhi ya wasanii lakini wao wameonesha kuwa wanaendesha maswala yao ki office na sio ki mtu binafsi ndio mana unaona msanii ambaye ana tatizo nao hawamuhusishi na chochote katika program zao.

Lakini hili limeonekana kuwa somo gumu kwa EAST AFRICA REDIO na hata TV ila zaidi likionekana kwa mtangazaji mmoja @dullaplanet.
@diamondplatnumz inajulikana toka mwanzo kuna vitu vilikuwa havimfurahishi ndani ya vituo hivi na hata mtu mwenye jicho la tatu angejua na haya yalikuwa yamejidhihirisha ndio mana sikuona ajabu hata kwa @diamondplatnumz kususia tuzo zao.

Naamini kususia kwake na @wcb_wasafi kwa ujumla ni kitu ambacho hawakukipenda EATV NA REDIO lakini walishindwa kujua kuwa ni mbegu ya zile firigisu walizokuwa wanazionesha mwanzoni na hata angekuwa nani asingeshiriki.

Kitu ambacho nimekishangaa kwanza wamefungia nyimbo za msanii yoyote wa @wcb_wasafi nyimbo zake kuchezwa kwa kawaida nilijua watafata misingi ya @cloudsfmtz na @cloudstv kutojihusisha na chochote juu ya wasanii ambao wana tatizo nao ila wao wamekuwa wakiandaa mijadala ya kuwachafua wasanii wa @wcb_wasafi .

Mjadala wa kwanza ni wa @dullaplanet dhidi ya tuhuma kuwa diamond kasema hategemei media kwenye kazi zake.Ulianzishwa mjadala wa kupotosha watu kuwa diamond haheshimu vyombo vya habari kitu ambacho sio kweli lakini @dulla na #djsummer walianzisha mjadala na kushutumu vikali jambo ambalo halina ukweli.
Ila tukaona juzi ikaandaliwa interview yenye lengo la kumchafua diamond akihusishwa #menejamaneno ambaye alitumia kipindi hicho kumtuhumu diamond kuwa ni msanii mchawi zaidi ambaye ashawahi kuwa chini yake.Interview ilijaa mada ya uchawi wa diamond zaidi kuliko wasanii wengine.Ila kilichonisukuma kuandaa makala hii ni kukosa uzalendo kwa wenzetu hawa @dullaplanet na @jr na kutaka kubadilisha nyeupe kuwa nyeusi kwa kuandaa mjadala na uchambuzi kuwa @rayvanny hakuwa nominated tuzo za #BET.Nikawa najiuliza hawa wanajua weledi wa kazi zao wanaenda hewani kuongea vitu ambavyo hawana uthibitisho navyo.

KWANINI WASIOMBE RADHI.
By @abby1_thebest
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad