Issue ya John Bocco na Okwi Kusaini Simba...Hans Poppe Aanika Mambo Yote Hadharani..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Mabingwa wa Kombe la Shirikisho nchini Simba SC, Zakaria Hans poppe amekanusha timu yake kuwasajili wachezaji Aishi Manula, John Bocco, Shomari Kapombe pamoja na Emmanuel Okwi na kusema taarifa hizo ni za uongo.

Hans poppe amebainisha hayo baada ya kuenea kwa tetesi kuwa timu hiyo imeshawasajili wachezaji hao baada ya msimu 2016/2017 kuisha hivi karibuni.

“Ni uongo kusema kuwa sisi tumeshaingia mkataba na mchezaji yoyote maana hadi sasa mikataba ya wachezaji bado haijamalizika, tukisajili mtu sasa itakuja kuwa kama suala la Kessy ambalo tuliwaambia Yanga lakini wakajifanya wajuaji, matokeo yake wametema milioni 50 tena kwa huruma yetu” alisema Poppe.

Pamoja na hayo, Hans poppe amesema kwa sasa hawezi kusema chochote kama wameanza mazungumzo na wachezaji hao wanaotajwa zaidi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad