Mume Ainyonga kwa Mtandio Baada ya Kugombana na Mkewe..!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwanamume aliyefahamika kwa jina la Luhende Lusangija (34) mkazi wa Mwinamila Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga amekutwa amejinyonga nyumbani kwake kutokana na kile kilichotajwa kuwa mke wake alikuwa anauza mali za familia kutokana na mikopo aliyokuwa anadaiwa. 

Tukio hilo limetokea Jumamosi Juni 3,2017 majira ya saa 11 alfajiri ambapo marehemu akiwa na watoto wake watatu nyumbani, aliamka na kisha kuchukua mtandio huku watoto wake wakiwa wamelala, na kuamua kujitundika kitanzi sebuleni, na kusababisha kifo chake papo hapo. 

Mashuhuda wa tukio hilo walisema Mwanamume huyo amejiua kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni ugomvi wa siku nyingi na mke wake ambaye siku kabla ya tukio alikuwa ameshaukimbia mji wake. 

Wakisimulia tukio hilo majirani zake Safina Javali, alisema marehemu alikuwa na ugomvi na mkewe muda mrefu ambapo kila siku walikuwa wakipigana, kwa madai kuwa mwanamke alikuwa akikopa mikopo, na baada ya kushindwa kuirejesha alikuwa akiuza vitu vya ndani wakati mumewe akiwa safarini kwenye majukumu yake ya kikazi. 

"Juzi alipokuja mwanamume kutoka safarini akakuta kitanda kimefungwa kwenda kuuzwa, ili mwanamke alipe deni la mikopo aliyokuwa akiichukua, ndipo ugomvi mkubwa ulipozuka hadi kusababisha mwanamke kuukimbia mji wake na kwenda kusiko julikana", alisema Javali.

Akiongea kuwa baada ya tukio hilo kutokea walimsikia mtoto wake wa miaka 7 majira ya saa moja asubuhi akilia kwa uchungu na kupiga kelele, kuwa baba yake amekufa kwa kujinyonga na walipofika kwenye nyumba na kuchungulia mlangoni ndipo wakamuona amening'inia kwenye paa la sebuleni akiwa ameshafariki.

Naye mwenye nyumba Halima Issa ambapo marehemu alikuwa mpangaji wake, alisema mji huo ulikuwa na ugomvi mara kwa mara na walikuwa wakiwasuluhisha lakini ugomvi wao ulikuwa pale pale, na walipopata taarifa ya kifo chake walifika eneo la tukio kisha kuwasiliana na uongozi wa mtaa ili kufuata taratibu za kisheria.

Aidha Mwenyekiti wa mtaa huo wa Mwinamila Ngokolo mjini Shinyanga Yohana Munisa, alikiri kupokea taarifa za marehemu huyo majira ya saa moja asubuhi, na alipofika eneo la tukio alimkuta Lusangija akiwa tayari amejinyonga, ndipo akatoa taarifa polisi ambapo nao wakafika ili kuuchukua mwili wa marehemu.

Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Elias Mwita alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, huku ndugu wa marehemu wakitafutwa ili kuuchukua mwili huo kwa taratibu za mazishi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad