Ukweli Mchungu..Rufaa ya Kambi Rasmi ya Upinzani Dhidi ya Adhabu ya Mdee na Bulaya ni Hopeless na ni Kupoteza Muda Tu..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kuna taarifa kuwa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wamekata rufaa kupinga adhabu waliyopewa Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya (CHADEMA). Wabunge hao wamefungiwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa kipindi cha miezi kumi. Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, Toleo la 2013, Wabunge hao watapokea nusu mshahara na nusu posho kwa kipindi chote cha adhabu yao.

Rufaa hiyo, kama ipo kweli, ni hopeless, kupoteza muda na haitafanikiwa. Kuna sababu mbili za kisheria na kiuhalisia. Kwanza, Kanuni za Bunge hazina neno 'rufaa' au 'rufani'. Yaani, hakuna suala la rufaa kwa jambo lolote linaloamuliwa na Bunge (niko tayari kurekebishwa). Katika adhabu zinazotolewa na Bunge, kwa mujibu wa Kanuni ya 74 ya Kanuni za Bunge, hakuna rufaa inayozungumziwa.

Kukosekana kwa kifungu maalum katika Kanuni za Bunge kinachohusu rufaa dhidi ya adhabu kwa Wabunge ni pengo kubwa kisheria katika kuwasilishwa, kusikilizwa na kuamuliwa kwa rufaa hiyo inayosemwa kuwasilishwa. Bunge, au Mamlaka iliyopelekewa rufaa, haliwezi kuwa 'moved' kuifanyia kazi rufaa hiyo kwakuwa hakuna kifungu kinachoruhusu hilo.

Kiuhalisia, Mamlaka zote za Kibunge yaani Spika, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge walishiriki katika mchakato mzima wa kufikia uamuzi huo dhidi ya akina Mdee. Ndiyo kusema, mamlaka zote za Kibunge haziko 'huru' kupokea na kusikiliza rufaa hiyo na kuitolea uamuzi wa haki. La nyongeza ni kuwa wote wanatoka chama kimoja-chama tawala.

Katika hali kama hiyo, it is advisable to resort to judicial review as opined by Hon. Tundu Lissu if deemed necessary. Kwa Bungeni, mambo hayo yalishaisha.

Credit - Petro E. Mselewa ,JF
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad