DAH!! Bweni la Shule ya Sekondari Laungua Moto...Wanafunzi 18 Wajeruhiwa....

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wanafunzi 18 Wa Shule Ya Sekondari Philip Mangula Iliyopo Kata Ya Imalinyi Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe Wamejeruhiwa Katika Ajali Ya Moto Iliyotokea Julai 30  Majira ya saa moja jioni na kuteketeza mali zenye thamani ya milioni 45.

Mtendaji wa kijiji cha Kinenulo Martini Mwalongo amesema kuwa chanzo chamoto huo hakijajulikana na kwamba moto huo umetokea wakati wanafunzi wakifanya ibada katika vyumba vya madarasa huku milango na madirisha katika mabweni yaliyo ungua vikiwa yamefungwa.

Baadhi ya wanafunzi wameiambia ITV kuwa mabweni yaliyoungua ni matatu yote yakiwa ni ya wavulana  huku wazazi wakiiomba serikali kuhakikisha chanzo cha moto huo kinafahamika haraka.

Katibu tawala wa mkoa wa Njombe Jackson  Saitabau amefika shule ya  sekondari Philip Mangula mapema asubuhi na kuagiza wanafunzi kuendelea na masomo na kwamba halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa wakiendelea kufanya tathmini ya mali zilizoungua na vikiwemo vifaa vya wanafunzi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad