RC Geita Amzuia Waziri Kuzindua Filamu Yenye Utata ya Magwangala......

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Uzinduzi wa Filamu ya Magwangala  ambayo imechezwa na wasanii wa Mkoani  Geita pamoja na viongozi wa Halmashauri ya Mji   ulikuwa ufanyike siku jana (Julai 27) umekwama kutokana na kuwepo kwa madai ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kulalamika kuwa filamu hiyo inaonekana kuwa na mahudhui ya  uchochezi baina ya wananchi na mgodi Mkoani humo.

Uzinduzi  huo ulitarajia kufanywa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura katika ukumbi wa Desire Park .

Akizungumza  juu ya hatua ya kukwama  kwa uzinduzi huo Naibu Waziri  Wambura, amesema kuwa kilichotokea alipatiwa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa kwamba kuna picha ambayo sio nzuri na kwamba wao kama mgodi walilalamika juu ya picha hiyo na kwamba wameangalia na kuona kuwa kuna maeneo ambayo yamerekodiwa sio mazuri na tatizo ni mawasiliano baina ya Afisa utamaduni na Mkoa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha wasanii  Mkoani Humo ambaye pia ni moja kati ya wachezaji wa Filamu Hiyo  Bi, Rosemery Michael, amesema kuwa wao hawakuona mapungufu yoyote kwa maigizo ambayo wameigiza kwenye filamu hiyo ni uhalisia wa maisha ambayo yapo ndani ya Mkoa husika.

Baadhi ya wasanii na wananchi ambao wameudhuria siku ya jana kwenye uzinduzi wa Filamu Hiyo, Sagari Mganga na Neema Philipo wamesema kuwa hata wao wameshindwa kujua ni maswahibu gani ambayo yamejitokeza ambayo yamesababishwa filamu hiyo kutokuzinduliwa.

Manase Ndoroma ni meneja mwandamizi wa mgodi  ambaye anashughulika na maswala ya jamii, ndani ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita  (GGM)  amefafanua kuwa wao  hawana ugomvi na sanaa wala na wasanii ila kumetokea shida ambayo wametoa kwa jamii kwa makusudi na kwamba mgodi huo una athari kwa jamii ambayo inauzunguka.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huo ndio ukweli SI akasia Tu ambao tuna mgogoro Ni wote wizi. Ashant na GGM Wote mko kapu moja na nyinyi ndio zaidi kabisa manake mpaka ndege zenu zinatorosha mkisaidiwa na baada ya wakati WA nchi hii. JIPANGENI NA MUWE WAKWELI NA TUTAHAKIKI KAMA ILIVUO KWA BRADLEY NA CREW. MNATUIBIA SANA

    ReplyDelete

Top Post Ad