VIDEO: Diva Awachana Watangazaji wa Clouds FM, Kisa Malinzi wa TFF

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mtangazaji wa kipindi cha Ala Za Roho cha Clouds FM, Diva The Bawse ameamua kutoa yake ya moyoni kwa kuwachana watangazaji wenzake ambao wamekuwa wakimzungumzia vibaya baba yake mzazi ambaye ni rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi.



Akiongea na Bongo5, Diva amesema, “Nimeipokea vibaya sana habari za baba yangu Jamal Malinzi kuingia katika matatizo, nilishtuka unajua siku hizi kila kitu unaona kwenye mtandao eeh, nikaamua niende nyumbani.”

“Hili suala linaniuma sana, kuna watu wengine mimi ninafanya nao kazi lakini niamini wanafurahia sana wanatuma vitu katika mitandao ya kijamii, Instagram, Facebook za kumzungumzia baba yangu vibaya halafu najiuliza mimi huyu nafanya naye kazi alafu anafanya hivi yaani hana hata utu najisikia huzuni sana,” ameongeza.

Mtangazaji huyo ameendelea, “Namuombea kwa Mwenyezi Mungu, mimi na familia yangu na siku hizi tunaenda kanisani kila siku St Peters ili haya matatizo yapite kwa sababu mimi nina wadogo zangu ambao wao ndio wanao athirika zaidi.”

“Unajua wakati mwingine upo katikati ya kipindi unakuta mtu anakupiga komenti kama tatu hivi anazungumzia mambo hayo unajua hali unayoipata eenh, inakuuma kwa sababu yeye amenilea nimeishi naye nyumba moja, amenipa kila kitu ninachotaka. Amenipa elimu na kila kitu ninachotaka alafu unaona vile vitu vinaendelea tena mtu ambaye unafanyanae kazi anafurahia na anaposti na video lakini familia yangu inaniambia niwaache ila kwangu mimi atabaki kuwa baba bora,” amesisitiza.

“Baba ametuambia watoto wote hamna kwenda kumuona bali tumuombee na tujitume zaidi katika kutafuta maisha ila kaka yangu anakwenda kumuona.”
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad