AGNESS Masogange yamkuta ya Wema

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mkemia kutoka Ofisi ya Mkemia mkuu wa Serikali amesema mkojo wa mrembo Agness Gerald 'Masogange' umekutwa na chembechembe za dawa za kulevya aina ya heroine na oxazepam (Diacety Imophine).

Mkemia Elias Mulima (40) ameiambia mahakama mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kwamba sampuli ya mkojo wa Agness zilizowasilishwa kwao zilikua na chembechembe za dawa za kulevya.

Mulima ambaye ni shahidi wa kwanza katika kesi ya Masogange kukutwa na dawa za kulevya Februari 15, 2017 Dar es salaam akiongozwa na Wakili wa Serikali Constantine Kakula, Shahidi huyo amedai kuwa Februari 15 mwaka huu katika ofisi ya Mkemia mkuu Dar es salaam akiwa ofisini alipokea vielelezo kutoka Jeshi la Polisi vilivyowasilishwa na koplo Sospeter na WP Judith kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi ili kubaini kuwa ni dawa za kulevya au la.

Pia shahidi huyo ameongeza kwa kudai kuwa iliwasilishwa na fomu maalumu ya dawa za kulevya ambayo ilikua na namba DCEA 008 na alifanya usajili na kuipa namba ya maabara 446/2017 ambapo Mshtakiwa alipewa kontena maalumu kwa ajili ya sampuli ya mkojo.

Pamoja na hayo Wakili wa utetezi Nehemiah Nkoko alipinga kupokelewa kwa kielelezo hicho kwa sababu Polisi walitakiwa kuiomba Mahakama ili wachukue vipimo vya Mshitakiwa lakini hawakufanya hivyo na kudai ni kinyume na sheria 63 CPA.

Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 28/2017  ambapo siku hiyo inatarajiwa kutoa uamuzi wa kupokea ama kutopokea vielelezo vya sampuli ya mkojo wa Agnes Masogange kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad