Maskini Sumaye Afunguka Haya 'Sirudi CCM Pamoja Kuwa Natateseka Kwa Visasi na Kunyang'anywa Mashamba yangu yote'

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

"Mmeamkaje? Kwangu mambo siyo mazuri. Mtakumbuka baada tu ya kuingia upinzani serikali ilitishia muda mrefu kuchukua mashamba yangu bila sababu za msingi, hata wakati wa kampeni baadhi ya viongoz wa ccm walitamka hadharani kuwa huyu dawa yake ni kumnyang'anya mashamba yake. Shamba la mabwepande ekari 33 wameagiza wiki hii halmashauri iligawe kwa wavamizi na wengineo.

Jana nimepokea barua kuwa shamba la mvomero ekari 326 limetwaliwa na rais na sitakiwa kukanyaga hapo. Shamba hilo lina majengo, mazao, mashine mbali mbali, visima virefu vya maji, umeme na mifugo mchanganyiko zaidi ya 200. Kisingizio shamba halijaendelezwa! Shamba lenye vitu vyote hivyo halijaendelezwa??

Mbaya zaidi katika kupinga dhamira hizo nilifungua kesi mahakama kuu kwa mashamba yote na mahakama zimeweka zuio la kutokuingiliwa mashamba hayo mpk mashauri ya msingi yatakapoamuliwa.

Lakini wameshaamua kwa hiyo mahakama hazina kazi. Utawala huu haufuati sheria ni udikteta mtupu! Kuna mwana ccm moja alisema "tutamfilisi mpk atakapotembelea ndala ndo atakumbuka kurudi ccm."

Hilo litawezekana kama Mungu huyu ni wa ccm. Ccm sirudi pamoja kuwa najua nitateseka na familia yangu! Kisasi hiki mimi sitakiweza namwachia Mungu ndiye atakayetufuta machozi mimi na familia yangu."

FREDRICK TLUWAY SUMAYE.
WAZIRI MKUU MSTAAFU.


Source: JF
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mashamba yote hayo uilkuwa umejimilikisha leo unaanza kulalamika pole sanaaaaa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Siyo kujimilikisha kama mtanzania ana haki kumiliki ardhi ,kwa nini wasiyachukue wakati yukk kwao? Usihudhunike mzee wangu yatakwisha 2020

      Delete
  2. Baba Zero tena ni wa kishtakiwa kwa utumizi mbaya wa Madaraka na kujimililisha Aedhi pasi na uhalali. na kama anavyo dai kuma mifugo jua tutakuja kupiga mnada .. magumashi bado unajiita waziri mkuu mstaafu. juoni haya na ilikuwa kwa vigezo gani mpaka ukabebwe..tena usingoje mpaka tukupitie anza kurudisha na kariakoo kodi ya lulipa huna na ...YRA WAKO KAZINI

    ReplyDelete

Top Post Ad