Mkojo wa Wa Manji Wazidi Kuleta Utata Mahakamani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mkojo wa Wa Manji Wazidi Kuleta Utata Mahakamani
WAKILI wa utetezi katika kesi inayomkabili mfanyabiashara Yusuf Manji ya kutumia madawa ya kulevya, Hoodson Ntisiepo, amemuuliza mtoa ushahidi kutoka ofisi ya mkemia mkuu wa serikali iwapo mkojo alioupima ulikuwa ni Manji au wa polisi?

Hayo amehoji leo Jumatano, Agosti 23 katika Mahakama ya Kisutu, wakati wa kusikilizwa kwa ushahidi wa kesi hiyo.
Wakili huyo alihoji jambo hilo ili mashahidi waithibitishie mahakama kwani wakati Manji anakwenda msalani kutoa sampuli hiyo ya mkojo aliongozana na askari, jambo ambalo lilifanya wasikilizaji wa kesi hiyo waangue vicheko ndani ya mahakama.

Kesi hiyo ilikuwa imekuja kwa ajili ya kutolewa ushahidi na imeahirishwa hadi Agosti 25 mwaka huu ambapo Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Cyprian Mkeha atakapotoa uamuzi kama mshitakiwa ana kesi ya kujibu ama la.

Ofisa kutoka ofisi ya mkemia wa serikali ambaye alikuwa akitoa ushahidi wake ameelezea namna alivyopima mkojo huo na kugundulika kuwa na chembechembe za madawa aina ya heroine ambapo.
Pia aliieleza mahakama kuwa majibu ya vipimo hivyo yanaweza kutokana na matumizi mbalimbali ya dawa zikiwemo dawa za binadamu za usingizi.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wacheni uonevu na visasi visivokuwa na msingi mykae mukijua malipo ni hapa duniani munamuonea hamna lolote nendeni mukawakamte wenye kutumia hasa

    ReplyDelete

Top Post Ad