Sumaye Afichua Siri Nzito za CHADEMA Kukabiliana na Magufuli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

HATIMAYE Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimefichua siri nzito kwamba kina program maalum kwa ajili ya kupambana na kandamizaji wa demokrasia unaofanywa na Rais John Magufuli

Siri hiyo imedokezwa kwa MwanaHALISI online leo na Mjumbe wa Kamati Kuu Frederick Sumaye.

Sumaye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani ya Chadema, alisema chama hicho hakijakaa kimya kama inavyoonekana na kwamba ipo program maalum ambayo anaamini itasaidia kupambana na ukandamizaji huu.

”Kama Rais Magufuli hataki sisi tufanye siasa ni aje ni mapngo maalum wa kufuta mfumo wa vyama vingi hapa nchini,” alisema.

”Lakini ilimradi hathubutu kufuta vyama vya siasa ni lazima tuendelee kufanya siasa,” amesema Sumaye.

Amesema program hiyo inaratibiwa na chama na kwamba muda siyo mrefu anaamini kwamba wataendelea kufanya siasa hapa nchini.

Ameongeza kuwa licha ya kuwapo program hiyo ya kukabiliana na matatizo haya ya ukandamizaji wa demokrasia unaofanywa na Rais Magufuli, lakini pia italenga kukieneza chama kwa Watanzania.

Sumaye ambaye alishika nafasi ya Uwaziri Mkuu kwa miaka 10 mfululizo, amesema hawapo kimya na kwamba pale wanapominywa watahakikisha wapaza sauti zao kwa kusema.

Kuhusu Madiwani wa Chadema kuhamia CCM, Sumaye amesema siasa hizo zimepitwa na wakati na kwamba kinachotakiwa kufanywa na CCM siyo kurubuni viongozi wao na kuwachukua bali kufanya vitu ambavyo vitawavutia Watanzania wakipende.

”Kazi inayotakiwa kufanywa na CCM ni kuimarusha chama hicho na siyo kuchukua madiwani ama viongozi wengine kwa kudhani kwamba ndiyo wanadhoofiha vyama vingine vya upinzani.

Amesema CCM kwa sasa hakifanyi siasa bali kinajivunia dola ambayo inawabeba na kwamba mwaka 2020, lazima kiondoke madarakani.

”Badala ya kutatua matatizo ya wananchi wao wananunua madiwani ili kionekani kina nguvu,” amesema
Kinachofanya chama kiwe na nguvu ni kutatua matatizo ya watu na kwa sasa watu wanaogopa kusema kwa sababu ya hofu ya dola na siyo kitu kingine.

Kuhusu kudumisha umoja wao wa Ukawa, Sumaye amesema wana mipango mingi ili kuhakikisha wanamsaidia, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad.

Amesema lengo serikali kumsaidia Ibrahim Lipumba ni kutaka kudhoofisha chama hicho pamoja na Ukawa na kwamba wamegundua hilo na wamejipanga kukabiliana nalo.

Ameongeza kuwa lengo ni kumdhoofisha Maalim Seif kwa sasabu wanajua CCM haiwezi kushinda uchaguzi kwa upande wa Zanzibar.

Jamii Forums
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Baba Chero..!! Bado upo HAI au Alusha.. Tupe Sera zako kabla ya Lukuvi kuwadia ili tuzitafakari.. Hapa Kazi Tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad