Heche Awatupia Lawama Polisi Kumchukua Kubenea Hospitali Kwaajiri ya Kuhojiwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Heche Awatupia Lawama Polisi Kumchukua Kubenea Hospitali Kwaajiri ya Kuhojiwa
Mbunge wa jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, Saed Kubenea ameshindwa kuhojiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge kufuatia hali yake kuwa mbaya na kulazwa katika Dispensary ya bunge mjini Dodoma.

Kubenea alikamatwa na polisi jijini Dar es Salaam jana na kupelekwa Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama  ya Bunge lakini ameshindwa kuhojiwa kufuatia hali yake kiafya kutokuwa nzuri jambo lililopelekea kulazwa.

Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche amethibitisha hilo na kulilaumu jeshi la polisi kumkamata Saed Kubenea akiwa hospitali ili tu aende kuhojiwa Dodoma.

"Baada ya Mhe. Kubenea kufikishwa Dodoma ameshindwa kuhojiwa kwasababu imethibitika anaumwa sana na sasa yuko Dispensary ya bunge amelazwa. Ni aibu kwasababu inatumika nguvu kubwa na gharama bila sababu ili tu kuwaumiza wabunge wa upinzani. Polisi wanamchukua mbunge kutoka hospital kisa wito wa kamati ambayo maamuzi yake ni mwezi wa kumi na moja, vitendo hivi vya kinyama tunavyofanyiwa hata serikali za wakoloni hawakuwafanyia watu weusi" alisema John Heche

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad