Jaku Ayoub Amtaka Spika Kuteua Wabunge wa Kwenda Kumjulia Hali Lissu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jaku Ayoub Amtaka Spika Kuteua Kuteua Wabunge wa Kwenda Kumjulia Hali Lissu
Mbunge wa Baraza la Wawakilishi (CCM), Jaku Hashim Ayoub ameomba mwongozo wa Spika akitaka Bunge liteue wabunge wa kwenda kumuona mwenzao wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu anayepata matibabu mjini Nairobi, Kenya baada ya kujeruhiwa kwa risasi.

Lissu alijeruhiwa Septemba 7 akiwa ndani ya gari nyumbani kwake Area D mjini hapa na alisafirishwa siku hiyohiyo kwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi. Awali, alipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza baada ya kipindi cha matangazo ya wageni bungeni leo Jumatatu, Jaku amesema Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alifanya kitendo cha kibinadamu kuruhusu gari la ndugu zake limpeleke Lissu hospitali.

Amesema kwa ubinadamu, anaomba mwongozo wa Spika wateuliwe wabunge kwenda kumuona Lissu.

Dk Tulia akijibu mwongozo huyo amesema wapo wabunge Nairobi ambao humletea taarifa Spika kila wakati juu ya hali ya mbunge Lissu.

Amewataja wabunge hao kuwa ni Freeman Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai na  Mwenyekiti wa Chadema, pia Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.

Mwingine ni Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa.


----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jaku... ukiwa utatumia wakati wako na kwa gharama zako binafsibasi haina haja hata kulizungumzia.
    Kila anae taka anafanya kivyake vyake
    kwa wakati wakNa kwa Gharama zake.
    Fokira yako ni nzuri ila si mahala pake.
    Mbatia aliumwa . lowassa mgonjwa. sumaye mgonjwa. ndiyo hali ya kibinadamu na maisha.
    wala huyolaumiwa kama hukujaaliwa kwenda. muombe sala ya uzima kama gwajima.

    ReplyDelete

Top Post Ad