Lissu Akipona Atatusaidia Kukamilisha Upelelezi- Mwigulu Nchemba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Lissu Akipona Atatusaidia Kukamilisha Upelelezi- Mwigulu Nchemba
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amezungumzia uchunguzi wa tukio la kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu akisema anaamini akipona atatoa mchango mkubwa katika upelelezi.

“Lissu tunamuombea akishapona atatupa mchango mkubwa wa kusaidia uchunguzi, mtu akiwa kwenye maumivu makali huwezi kumuuliza lolote,” amesema Mwigulu akizungumza leo Alhamisi katika kipindi cha Clouds 360.

Amesema kutokana na upya wa uhalifu wa aina iliyotokea kwa Lissu, kuna mambo wanaendelea kuyafuatilia ambayo hawezi kuyaeleza kwa sasa.

“Suala la Lissu kutokana na upya wake, kuna vitu tunaendelea kuvifuatilia, hivyo kuna mambo hatuwezi kuyasemea,” amesema.

Amewataka Watanzania waendelee kuwa na subira kwa kuwa kazi inaendelea kufanyika.

Mwigulu amesema baada ya tukio la kushambuliwa Lissu Septemba 7, taarifa kadhaa zilichukuliwa eneo la tukio ambazo zinaendelea kufanyiwa kazi ili kupata undani wake.

“Wahalifu hawajakamatwa wote, ukianza kusema itakuwa ni shida, kuna mambo yanaendelea kufanywa na hayana ukomo. Ukomo utafikiwa endapo wote waliohusika watakamatwa. Nikisema naweza kuvuruga kazi inayoendelea,” amesema.

Akijibu swali la mtangazaji wa kipindi hicho kuwa watu wanahoji kwamba askari wanapouawa wahalifu wanakamatwa mapema Mwigulu amesema, “ Watu wakiwaza hivyo watakuwa wanakosea, hatuweki madaraja, ni mazingira ya tukio tu.”

Akizungumzia uchunguzi unaoendelea kuhusu kuvamiwa kwa Lissu amesema hawezi kueleza waliokamatwa bali tayari kuna magari zaidi ya 10 yanayofanana na lililohusika kwenye tukio yamekamatwa.

Mwigulu amesema alimuona Lissu siku ya tukio Septemba 7 akiwa katika Hospitali ya Rufaa Dodoma na baadaye uwanja wa ndege aliposafirishwa kwa ajili ya matibabu jijini Nairobi nchini Kenya ambako yuko hivi sasa.

Amesema hajafika Nairobi kumjulia hali Lissu bali kwa Mkoa wa Singida, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amefika.

“Katika mazingira mengine tunaendelea kupata taarifa, kama Serikali tuna balozi,  kama waziri kwenda kumuona ni jambo jema katika utaratibu wa uchunguzi hata dereva tutazungumza naye,” amesema.

Amesema dereva hivi sasa anapata tiba ya kisaikolojia na anaamini atakapokuwa tayari atazungumza na wanaokusanya taarifa.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad