Mr. Chuz Atoa Siku 14 kwa Chama cha Waigizaji Kumuomba Radhi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mr. Chuz Atoa Siku 14 kwa Chama cha Waigizaji Kumuomba Radhi
MKONGWE wa filamu Bongo anayewika na Tamthilia ya Closed Chapter, Tuesday Kihangala ‘Mr. Chuz’ ametoa siku 14 kuombwa radhi na Chama Cha Waigizaji Tanzania kutokana na kuchafuliwa kuwatumia kingono wasanii wa kike, wenye tamaa ya kuchomoka kisanaa.
Akizungumza na Ijumaa, Chuz aliyewika na Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu alisema kuwa, anasikitishwa na chama hicho kikubwa kutoa tamko kwenye vyombo vya habari kwa jambo la wazi lililo pangwa na genge la watu wachache.

“Nawapeleka mahakamani wale wasichana na mvulana alierekodi sauti ya kunichafua kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii, tayari mwanasheria wangu ameshakamilisha taratibu zote na muda wowote kuanzia sasa nitawafikisha mahakamani.
“Najua ni njama zilipangwa kunichafua na siku chache baadae baadhi yao walinieleza mipango yao ililenga nini na aliepanga mpango huo wamemtaja tena kwa ushahidi wa sauti, lakini pia nakipa Siku kumi na nne chama cha waigizaji taifa kiniombe radhi kwa ushiriki wao wa kunichafua,” alisema Chuz.

Mr. Chuz.
Ijumaa lilimtafuta kiongozi wa tume iliyounda kutoka chama hicho ambaye pia ni msanii wa filamu, Michael Sangu ‘Mike’ na alipopatikana alisema;
“Nilikuwa mwenyekiti tu wa kamati iliyoundwa kumhoji Chuz, watuhumiwa kipindi hicho walikuwa wawili, Jumanne Mshindo (aliyerekodi video chafu) na Chuz. Tulishindwa kumfikia kwa kuwa alikuwa Lushoto huko Tanga, kama ameamua kwenda mahakamani ataushtaki umoja wa filamu siyo mimi.”
Hivi karibuni, Chuz alikwaa skendo ya kutoka kimapenzi na wasanii wake ambapo sauti ilisambaa ikieleza jinsi anavyowadhalilisha wasanii wa kike ambao wanakataa kutoka naye.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad