Rais wa Zanzibar Dkt. Shein Amefanya Uteuzi wa Majaji wa Mahakama Kuu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais wa Zanzibar Dkt. Shein Amefanya Uteuzi wa Majaji wa Mahakama Kuu
Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Kwa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 94(2) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984, Rais Shein amewateua Khamis Ramadhan Abdalla na Aziza Iddi Suweid kuwa majaji wa Mahakama hiyo.

Pia, amemteua Kubingwa Mashaka Simba kuwa Katibu wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mujibu wa uwezo wake chini ya Sheria ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 4 ya 2015, kama ilivyorekebishwa na Sheria Namba 4 ya 2017, Kifungu cha 10(a)(1).

Katika uteuzi mwingine, Rais Shein amemteua George Joseph Kazi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala  Bora anayeshughulikia masuala ya Katiba na Sheria.

Dk Shein chini ya kifungu cha 6(2) cha Sheria ya Shirika la Bandari Namba 1 ya 1997, amemteua Kapteni Juma Haji Juma kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad