TID Atangaza Nia ya Kugombea Ubunge wa Kinondoni 2020 Je Atamng'oa Mtuli?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

TID Atangaza Nia ya Kugombea Ubunge wa Kinondoni 2020 Je Atamng'oa Mtuli?
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Khalid Mohamed maarufu kama T.I.D, ametangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Kinondoni, kwenye uchaguzi ujao unaotarajiwa kufanyika mwaka 2020, na kumng'oa mbunge wa sasa wa jimbo hilo Maulid Mtulia.

Akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio, TID amesema sababu inayomsukuma kugombea nafasi hiyo ni kutokana na mbunge wa sasa kushindwa kulitimizia mahitaji yake jimbo hilo, hivyo atatumia nafasi hiyo kuhakikisha anamng'oa ifikapo 2020, kwa kuwa yeye anafahamu vizuri matatizo ya Kinondoni kutokana na kuwa mzawa wa mahali hapo.

Akiendelea kuzungumzia suala hilo, TID amesema iwapo atapewa dhamana ya kuliongoza jimbo hilo, atahakikisha anatatua matatizo yote yanayowakabili watu wa Kinondoni, likiwemo janga la madawa ya kulevya.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Balaa duniani!Muziki umeanza kukushinda nini dogo?Maana kwenye nchi nyingine kwa hizo scandals zako nyingi na kuwahi mpaka kufungwa jela hauna chance kabisa ya kuongoza au kuiwakilisha jamii kivyovyote vile kwani wewe tayari ni mfano mbaya ndani ya jamii lakini kibongo bongo watakupa nafasi hiyo na baadaye watajuta kwanini walikuchagua

    ReplyDelete

Top Post Ad