Chadema Yawatupia Maswali kwa IGP Sirro,Mwigulu Sakata la Lissu, Saanane na Nape

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Chadema Yawatupia Maswali kwa IGP Sirro,Mwigulu Sakata la Lissu, Saanane na Nape
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimehoji maswali kibao kwa  Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP), Simon Sirro kuhusu mambo yanayoendelea kwenye upelelezi wa Ben Saanane, Tundu Lissu na aliyemtishia Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.

Saanane ni Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye hajulikani aliko na Lissu ni Mbunge wa Singida Mashariki ambaye alipigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7 mwaka huu.

Katika mkutano na waandishi wa habari leo Ijumaa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema ameanza kwa kusema,  “Ni siku 695 tangu Mawazo(Alphonce) auawe, siku 326 tangu Ben Saanane apotezwe na watu wasiojulikana na leo ni siku 26 tangu Lissu afanyiwe jaribio la kumuua na mpaka sasa polisi hawajasema lolote, zaidi ya Nissan 8 na zimehifadhiwa kusikojulikana,”

“Leo tunapozungumza, viongozi mbalimbali wanaendelea kutishwa, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya anatishwa na watu wamemfuata nyumbani kwake, Josua Nassari ametishwa, Lema(Godbless) ametishwa,”

“Ben Saanane alitishwa na alitoa taarifa Kituo cha Polisi Tabata na kapotea, Lissu alitoa taarifa kwamba anatafutwa na yaliyotokea mnajua,”

“Hofu ni kubwa, maiti zaidi ya 17 zimeokotwa Coco Beach hakuna ‘seriousness’ kwa matukio,” amesema Mrema

“Waziri anatishwa mbele ya kamera na hakuna jitihada, IGP anasema hajui alipo, hii inaonyesha hakuna ‘seriousness’ katika kupambana,” amesema Mrema

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni wa Chadema, Kigaila Benson amesema, “Haya mambo si ya kawaida, yanafanywa na watu wasio wa kawaida, niseme tu hakuna aliye salama, hujui kesho yako,”

“Kuna kijana anaandika mambo ya ajabu, kwa nini polisi hawaoni, IGP anachagua mambo ya kusikia, kwa nini ukimkosoa Rais jioni yake unakamatwa,”

“Kama polisi wanaona, hawachukui hatua? Walipouawa polisi pale Mbagala, watu waliotuma picha walikuwa Mahenge, walikamatwa sasa huyu kijana anafanya nini?

“Wanasema wamekamata Nissan, hivi hizi Nissan zilikuwa wapi, zilikuwa zinaendeshwa na nani? Hii si ni kanya boya?

“Waziri Mwigulu anasema gari alilolitaja Lissu liko Arusha, waziri ametumia kigezo au kifaa gani kubaini gari halikuwahi kufika Dar? Kwa nini chombo hicho kisitumike kuwabaini waliomshambulia Lissu?

“Mwigulu kwa nini amechukua uwakili wa mtuhumiwa? Amehojiana vipi na huyo? Kwa nini mtu huyo anayetuhumiwa asikamatwe na sasa anafanya kazi ya kumtetea?

“Polisi wanatakiwa kutuambia, upo wapi usalama wa Rais,” “Tumesimama upepelezi wa tukio la Lissu kwa sababu ya dereva, ina maana kama dereva angekufa upepelezi usingekuwapo?

“Sisi hatuwezi kumficha dereva, anapata matibabu, ila kama wamesema wanafahamu gari lile lipo Arusha wanashindwaje kwenda kuzungumza na dereva,” amehoji Kigaila

“Sirro analitumia jeshi kisiasa, Sirro kwa nini asimuulize RPC Kaganda(Suzan) aliyekuwa Kinondoni ambaye alikuwapo siku Nape anatolewa bastola kwa nini hawakumkamata,”

“Jeshi la polisi ni letu sote, tusilitumie kisiasa, tunataka tueleweke kwamba IGP wanamjua huyu mtu,”

“Kwa nini wanamtafuta mtu ambaye walikuwa naye, hivi kwa nini maswali magumu wanakuwa na majibu ila maswali mepesi wanakosa majibu,”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad