Jafo Awabana Wadaiwa Sugu wa Bodi ya Mikopo Awataka Kulipa Kabla ya Desemba 30

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jafo Awabana Wadaiwa Sugu wa Bodi ya Mikopo Awataka Kulipa Kabla ya Desemba 30
Halmashauri 12 ambazo ni wadaiwa sugu wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa zimetakiwa kabla ya Desemba 30 ziwe zimerejesha deni la Sh2 bilioni.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo ametoa agizo hilo leo Alhamisi.

Halmashauri hizo ni Mwanza, Mbeya, Moshi, Singida, Kigoma, Karatu, Mbinga, Pangani, Mbinga, Morogoro, Igunga na Kongwa.

Jafo amesema hadi Septemba 30 bodi imetoa mikopo yenye thamani ya Sh9.7 bilioni kwa halmashauri 54 nchini.

Amesema hadi Septemba 30 fedha zilizorejeshwa ni Sh6.6 bilioni.

"Halmashauri nyingi zimejitahidi kurejesha mikopo kwa wakati lakini kuna zilizoonyesha usugu katika kurejesha mikopo," amesema.

Amesema kutorejeshwa kwa mikopo kunasababisha halmashauri nyingine kukosa fursa ya kukopa.

Jafo ameiagiza bodi kuangalia utaratibu wa kupitisha mikopo inayolenga ujenzi wa viwanda na uwekezaji katika halmashauri ili kukuza ajira na uchumi wa viwanda.

"Bodi iache kubweteka, ijipange kimkakati  kujenga uwezo mkubwa wa kutoa mikopo kwa halmashauri zilizo makini katika mapinduzi ya viwanda," amesema.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hongera Jafo.
    Asyerejesha anaingua katika Black book na uongozi unabasilishwa baada ya kuwafikisha katika mkono WA sheriaSHAMBA LA BIBI LILISHAUNGUA MOTO KABLA YA AWAMU HII. SASA HAPA NI KAZI HALALI NA UADILIFU NA SI VINGINEVYO.
    KAMA ILINUMUA NYUMBA ZA MALAZI TUTAZIUZA NA PESA ITARUDISHWA HILI LINAELEWEKA

    ReplyDelete
  2. Nadhani katika mawaziri wapya Jafo ni mmoja miongoni mwa wachache watakaokuwa na smooth transition.

    ReplyDelete

Top Post Ad