Jafo na Dkt Kigwangalla Watoa Neno Baada ya Kuapishwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jafo na Dkt Kigwangalla Watoa Neno Baada ya Kuapishwa
Aliyekuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI, Seleman Jafo baada ya kuteuliwa na kuapishwa kuwa Waziri wa wizara hiyo amewaahidi Watanzania kuwa wategemee utendaji mzuri wa kazi kutoka kwake huku akiwaomba watumishi wote umma kufanya kazi kwa spidi.

Wakizungumza Ikulu jijini Dar es salaam mara baada ya kuapishwa, Mhe Jafo amesema lengo lake ni kuisukuma nchi ifikie malengo yanayotarajiwa huku Dkt Kigwangalla akisema Mh. Rais ameonyesha imani kubwa sana na uwezo wake.

“Kikubwa zaidi niwaahidi Watanzani wategemee utendaji mzuri wa kazi, lakini niombe sana watumishi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lazima wajipange kufanya kazi kwa bidii , Wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya, Wakurugenzi naomba waongeze spidi na Wakurugenzi waongeze spidi lakini watumishi wote waongeze spidi lengo ni tuisukume nchi yetu ifike katika malengo tunayoyatarijia

Hata hivyo Mhe. Jafo alipoulizwa kuwa ikiwa ni miongoni mwa Waziri walipandishwa yeye anafikiri ni kwanini kapandishwa na kuwa Waziri kamili? Akijibu “Ni mipango ya mwenyezi Mungu jambo la kwanza, la pili ni imani ya Mheshimiwa Rais kwangu, tatu ni utendaji wa kazi kwasababu ni lazima popote utakapo niweka ni lazima nifanye kazi kwasababu nina dhamana ya Watanzania naamini popote Mungu ananiona.”

Kwa upande wake aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya ambaye kwasasa ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla amesema kuwa “nimefarijika sana pia nimepewa imani kubwa na Mhe. Rais, nimepewa Wizara nyeti ni wizara ambayo inachangia asilimia 17.2 ya pato la taifa ni wizara nyeti sana, na mimi kupewa jukumu hili maana yake mhe. Rais ameonyesha imani kubwa sana na uwezo wangu lakini pia na uzalendo nilionao naomba niwaambie Watanzania na Mhe. Rais Kuwa sitawaangusha.”
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tunawapongeza Waapishwa. Wizara zimepanguliwa na kuongezwa kutokana na uchambuzi uliofanyika na kuonekana iko Haja ya Sisi kuyafanya haya. Na tumeshayafanya .
    Tunacho tegemea na kuona ni Kwamba Ufanisi na Weledi wenu nchicho kilicho tupa msukumo mkubwa.
    Nia na Lengo Viko Wazi Ni Kumtumikia Mtanzania na Kuweza Kuboresha Maisha yake na Kumpa Huduma Stahiki kwa Wakati Stahiki na Bila Ulongo Longo.
    Kinacho wezekana leo KISILALE Na Bila Usumbufu kinafanyika Ili tuweze kuipeleka Tanzania katika Next Level.
    Imani Juu yenu tunayo Uadilifu wenu na Uzalendo wenu Hatuna shaka Nao.
    Tunawatakieni Kila la Kheri Katika Majukumu yenu Mapya na kumbukeni Dhamana mliyokabidhiwa ni ya Kumtumikia Mtanzania Bila Kujali
    Rangi Yake!
    Dini yake!
    Ukabila Wake!
    Chama Chake!
    Tanzania ndiyo Kwanza na UBUNIFU uwe ni Wndelevu.
    Ajira na Makazi iwe ni Kipa Umbele.
    HAPA KAZI TU..... Hongera Baba JPJM na Mh Kassim Majaliwa.

    ReplyDelete

Top Post Ad