AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Ulega aliyasema nayo wakati wa ziara yake aliyoifanya Wilaya ya Mkuranga-Pwani kwenye vijiji Vinne ,ambapo alisema hakuna sababu ya wananchi wa Mkuranga kuchukua Kuku mikoa mingine wakati wanaweza kufuga wenyewe na kujipatia kipato na maendeleo yakapatikana na kuwawezesha kuuza hata sehem nyingine.
Amesema yuko tayari kuwasaidia wananchi wa Mkuranga mbegu za Kuku pamoja na watalaam wa kuwafundisha jinsi ya kufanya ufugaji wa Kuku na samaki wa kisasa.
Amesema ajira katika Wilaya hiyo zipo ikiwa ni pamoja na ufugaji Kuku pamoja na samaki ambayo ni ajira ya kudumu na soko ni kubwa kutokana mahitaji ya vitoweo hivyo kuhitajika kwa wingi.
"Sioni sababu wananchi wa Mkuranga kuchukua kuku kutoka mikoa mingine wakati mnaweza kufanya nyinyi wenyewe kutokana na maeneo mlionayo, haitawezekana kama nyinyi hamtaweza kuonyesha mfano nikiwa ni Mbunge na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi"alisema Ulega.
Katika ziara yake alitembelea Ujenzi wa Zahanati za Kibamba, Kimazichana na Mwandege na kuahidi kuwaunga mkono wananchi katika juhudi mbalimbali wanazoonyesha katika maendeleo ya huduma za jamii.
Ulega amesema kuwa wakati uliopo ni kufanya kazi za Maendeleo kwa kuunga mkono jitihada za Rais Dk. John Pombe Magufuli juu ya dhamira ya serikali ya Viwanda.
Naibu waziri aliaahidi kuchagiaji sh. Milioni moja na mifuko ya saruji kwa ajili ya kikundi cha VICCOBA cha wanawake waliojenga ukumbi wa mikutano na sherehe kilichopo Mwandege.
Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.
Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA
Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK