Shonza kuanza na Wasanii Wanaovaa Vibaya na Kutumia Maneno Mabaya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza imetangaza kuanza kushughulika na wasanii ambao wanavaa vibaya na kutumia maneno mabaya kwenye kazi zao za sanaa.

Juliana Shonza amesema hayo leo alipokuwa anapokelewa ofisini na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harisson Mwakyembe na kusema alipoteuliwa tu aliona kuwa kwenye sanaa hususani wasanii wamekuwa wakivaa vibaya kwenye kazi zao na kutumia maneno yasiyo na maadili kwenye kazi zao hizo na kusema kama serikali lazima wahakikishe wanalifanyia kazi ili kulinda utamaduni wa Tanzania.

"Nilipoteuliwa tu ni jambo ambalo nilianza nalo ni mmomonyoka wa maadili kwa kweli imekuwa ni changamoto kubwa sana nimeshuhudia saizi hata ukiangalia kwenye nyimbo na kazi za sanaa lugha ambayo inatumika inakuwa siyo nzuri, lakini kama haitoshi kuna nyimbo ambazo zinaibwa ukifuatilia ndani unakuta maadili siyo mazuri, lakini hata katika suala la mavazi mimi nalisema wazi nitawaambia wasanii wa kike wajitahidi kuvaa vizuri, kwa sababu hatuwezi kuacha hivi vitu vikawa vinaendelea tu kila taifa na misingi yake na tamaduni zake" alisema Juliana Shonza

Mbali na hilo Naibu Waziri wa Habari amesisitiza kuwa ni jukumu la viongozi kuhakikisha utamaduni wetu unaendelezwa na kusimamia misingi ya taifa.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mama Shonza, mungu akubariki na hongera kwa uamuzi huu na nndiyo tunayo yataka. Maadili yetu ni lazima tuyagifadhi na vizazi vijye tanzania yetu na utamaduni wake.

    ReplyDelete
  2. Mama Shonza, mungu akubariki na hongera kwa uamuzi huu na nndiyo tunayo yataka. Maadili yetu ni lazima tuyagifadhi na vizazi vijye tanzania yetu na utamaduni wake.

    ReplyDelete

Top Post Ad