Amissi Tambwe Aanza Mkwara Akiwa Benchi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Amissi Tambwe Aanza Mkwara Akiwa Benchi
STRAIKA wa Yanga, Amissi Tambwe amesema hali yake kwa sasa siyo mbaya sana na muda wowote atarudi uwanjani, lakini amepiga mkwara kwa kusema anataka kufukuzana kwa ufungaji na mfungaji bora.

Emmanuel Okwi wa Simba ndiye anayeongoza kwenye orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu Bara akiwa na mabao nane, sasa Tambwe anasema akirudi uwanjani atahakikisha anamfikia.
Tambwe amedai anatamani sana Okwi asiongeze bao lolote katika kipindi hiki mpaka yeye atakapoanza kuitumikia Yanga.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Tambwe alisema anaamini akirudi uwanjani na asipopata majeraha tena basi ndani ya mechi tatu au nne anaweza kufikisha mabao nane yaliyofungwa na Okwi.

“Hali yangu kwa sasa siyo mbaya sana ninamshukuru Mungu naendelea vizuri lakini pia naomba ligi isimame kwa muda hata mechi yetu ijayo na Mbeya City natamani isiwepo ili niweze kupona vizuri.

“Nataka siku nikirudi niweze kuwa fiti zaidi tayari kwa kupambana na akina Okwi na wenzake ambao hivi sasa wanachuana kwa kuzifumania nyavu,” alisema Tambwe.

Tambwe anayesumbuliwa na goti bado hajaanza mazoezi lakini mwenyewe amedai ndani ya siku chache zijazo atarejea uwanjani huku akijitibu binafsi
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad