Kamati ya Maadili Yamuweka Kikaangoni Kubenea Ahojiwa kwa Kosa la Kutoa Kauli ya Kudharau Bunge

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kamati ya Maadili Yamuweka Kikaangoni Kubenea
Kamati ya  Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imemhoji  Mbunge wa Ubungo Mheshimiwa Saed Kubenea kwa kosa la kutoa kauli ya kudharau Bunge.

Akizungumza mara baada ya kumhoji Mbunge huyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Almasi Athuman  Maige (Mb) alisema, Mheshimiwa  Kubenea amefikishwa mbele ya Kamati  hiyo kujibu tuhuma inayomkabili kutokana na kauli aliyotoa kitendo ambacho   ni kinyume na kifungu cha 26 (e) na 34 (1) (a)   ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296.

Mheshimiwa Maige alisema mahojiano hayo yamefanyika  leo (jana) baada ya kuahirishwa mara mbili kutokana na Mheshimiwa Kubenea kutokua katika hali nzuri kiafya na hivyo kuomba mahojiano yaahirishwe.

Mheshimiwa Maige aliongeza kuwa  baada ya kumsikiliza Mhe. Kubenea itaandaa Taarifa yake na kuiwasilisha kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai kwa hatua zaidi.

“Kanuni zimeweka masharti kuwa shughuli za Kamati hii zinazofanywa zitabakia kuwa ni siri hadi hapo itakapomaliza kazi yake na kuwasilisha taarifa Bungeni,” alisema.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad