Kibatala : Lulu Anaweza Kupata Dhamana Akisubili Rufaa Kusikilizwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kibatala Atoa Ufafanuzi Kuhusu Dhamana Ya Lulu
WAKILI wa Elizabeth Michael ‘Lulu’, Peter Kibatala, kufuatia hukumu ya miaka miwili dhidi ya Lulu jana, ametoa ufafanuzi kupitia akaunti yake ya Instagrame kuhusu kitakachofuata alipoulizwa maswali na watu wengi ambapo alitumia fursa hiyo kuwafafanulia sheria inavyosema kuhusu nini kinafuata.

Majibu yake kwa maswali hayo ni yafuatayo:

Amesema kuwa hakuna hukumu tofauti inayoweza kutolewa kabla mhukukiwa hajatumikia theluthi ya kufungo chake ambacho kwa Lulu itakuwa ni kuanzia miezi  mitano.

Ndani ya hiyo miezi mitano dhamana inaweza kuombwa wakati wakisubiria rufaaa ianze kusikilizwa.  Kwa maana hiyo anaweza kutoka kwa dhamana muda wowote mahakama ikmpatia dhamana.

Huwezi kuacha kijana wa miaka 22 mwenye maisha marefu mbele yake ahukumiwe kwa uhalifu kwa sababu ya suala la muda, kwani itaharibu maisha yake ya mbele. Kwa hiyo rufaa imelenga katika kuondoa tatizo hilo.

Kukata rufaaa na kuomba dhamana  na kufanya kazi za jamii vinaweza kufanyika kwa wakati mmoja wakati suala hili likisubiriwa kusikilizwa na mahakama ya rufaa.

Ujumbe wa Kitabala katika Instagram ni ufuatao:



-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. jamani lulu miezi mitano mbona bado ni mbali sana

    ReplyDelete
  2. mi sijamuelewa (kibatala) naomba mliomuelewa mnieleweshe vizuri ina maana hata hiyo rufaa haiwezi kukatwa mpka atumikie theluthi ya kifungo chake???? au hata ikikatwa mapema itabidi isikilizwe baada ya hiyo miezi tano?

    ReplyDelete

Top Post Ad