Watetezi Haki za Wanyama Walaani Vifaranga Kuteketezwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Watetezi wa haki za wanyama wamelaani kuteketezwa vifaranga vya kuku 6,400 vilivyoingizwa nchini kinyume cha sheria.

Vifaranga hivyo mali ya Mary Matia (23), vyenye thamani ya Sh12.5 milioni vilikamatwa mpakani Namanga vikitokea nchini Kenya.

Kuteketezwa kwa vifaranga hivyo jana Jumanne Oktoba 31,2017 kumeibua mjadala ikielezwa kitendo hicho ni ukiukwaji wa sheria.

Kazi ya kuviteketeza eneo la Namanga wilayani Longido ilifanyika ikishuhudiwa na maofisa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Wizara ya Mifugo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.
Akizungumza wakati wa kuviteketeza vifaranga hivyo, ofisa mfawidhi wa kituo cha udhibiti wa magonjwa ya mifugo Kanda ya Kaskazini, Obedi Nyasebwa amesema kazi hiyo imefanyika kwa kuzingatia Sheria ya Magonjwa ya Wanyama namba 17 ya mwaka 2003. Pia, amesema Serikali mwaka 2007 ilitoa tangazo kupiga marufuku kuingizwa nchini vifaranga vya kuku na mayai.

Hata hivyo, watu mbalimbali wamehoji ulazima wa kuviteketeza vifaranga hivyo badala ya kuvirudisha vilikotoka kama alivyoomba mmiliki wake Matia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ustawi wa Wanyama (Taweso), Dk Thomas Kahema akizungumza na Mwananchi leo Novemba Mosi 2017 amesema anatambua dhamira ya Serikali ya kuzuia magonjwa ya kuambukizwa kutoka nchi jirani lakini kulikuwa na njia mbadala ya kufanikisha suala hilo.

Dk Kahema amesema mamlaka za Serikali zilitakiwa kuvirudisha vifaranga hivyo vilikotoka ili visieneze magonjwa kama inavyohofiwa.

Amesema kuviteketeza ni ukatili ambao hauungi mkono na kwamba, wanalaani kitendo hicho ambacho kinatoa taswira mbaya kwa Taifa linaloonekana halijali haki za wanyama.

“Zipo njia nyingi ambazo wangeweza kutumia mbali na kuchoma, mbona wakikamata ng’ombe hawawachomi moto?” amehoji Dk Kahema.

Amesema Sheria ya Ustawi wa Wanyama ya mwaka 2008 inasisitiza kutambuliwa kwa haki za wanyama, kwa hiyo kuteketezwa vifaranga hivyo kunaonyesha jinsi utekelezaji wa sheria unavyoibua utata.

Dk Kahema amesema vifaranga hivyo vingepimwa kubaini kama vina maambukizi na ingebainika havina vingetaifishwa au kugawiwa wajasiriamali, magereza au vituo vya watoto yatima.

Amesema hana uhakika kama sheria iliyotumika kuteketeza vifaranga hivyo inaeleza wazi kwamba viteketezwe.

Mkurugenzi mtendaji huyo amesema mamlaka hazikuweka wazi kama vifaranga hivyo vilikuwa na  maambukizi.

Amesema vifaranga havina hatia bali aliyevileta ndiye anayetakiwa kuchukuliwa hatua.

Baadhi ya wananchi kupitia mitandao ya kijamii wameonyesha kutoridhishwa na hatua iliyochukuliwa na mamlaka za Serikali wakieleza ni ukatili dhidi ya wanyama.

Abbas King ameandika kwenye ukurasa wa Facebook wa Mwananchi kuwa, “Hivyo vifaranga vina roho au vinaendeshwa kwa umeme? Kwa nini msivigawe kwa watoto yatima wakafuge vikue wafanye kitoweo, kama vina madhara virejeshwe kwao walioleta wapigwe faini.”

Tumaini Kyama ameandika katika ukurasa huo kuwa, “Swali langu ni kuwa kama alikuwa kachukua mkopo wa biashara huyo mmiliki wa hivyo vifaranga mkopo ataurudisha na nn sitaki kujua hayo mengine nimewaza kwa sauti tu. Tunapambana na umasikini au tunafurahia umasikini wa baadhi ya watu.”

“Ukiukwaji wa sheria ya wanyama na pia wamerudisha maendeleo nyuma. Vilevile hawajavipima vifaranga na kutufahamisha vina magonjwa gani na hata hivyo si wangevirudisha vilikotoka ili aliyevinunua arejeshewe fedha yake na kama ni faini apigwe ili iwe funzo kwa wafanyabiashara,” ameandika Lightdod Shayo.

  By Peter Elias, Mwananchi pelias@mwananchi.co.tz

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nasisi wananchi hebu tujifunze kufuata sheria ili kuepuka matatizo kama hayo, kitu ukiambiwa MARUFUKU basi na iwe MARUFUKU kweli, tusijaribu kuyapima maji kwa mguu..... au ndio kusema sheria zimewekwa ili zivunjwe? Ukibip-utapigiwa

    ReplyDelete
  2. Hebu punguzeni unafiki walau kidogo tu, vifaranga kuchomwa moto imekuwa nongwa , hivi kuku wangapi mnachinja na kuwala, mayai mangapi mnakaanga na chips? huko si kukiukwa haki za wanyama? kama ninyi ni wa kweli mbona hamkemei uwepo wa bucha na uvuvi wa samaki?, tule nyasi eti? shame on you!

    ReplyDelete

Top Post Ad