Zitto Kabwe Azitaka Taasisi za Uwajibikaji Ziachwe Kufanywa kwa Uhuru na Uwazi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Zitto Kabwe Azitaka Taasisi za Uwajibikaji Ziachwe Kufanywa kwa Uhuru na Uwazi
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo), Zitto Kabwe amesema licha ya Serikali kuonyesha juhudi za kukabiliana na rushwa, jitihada hizo hazitakuwa endelevu endapo taasisi za uwajibikaji hazitaachwa zifanye kazi kwa uhuru na uwazi.

Akizungumza katika mjadala ulioandaliwa na taasisi ya Twaweza leo Jumatano Novemba 29,2017, Zitto amesema taasisi kama Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG); Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA); kamati za Bunge za hesabu na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) zinapaswa kuachwa huru ili zifanye kazi kwa ufanisi.

Mjadala huo umelenga kuangalia ni namna gani ufa uliopo kati ya nia ya Serikali ya kupambana na rushwa kwa uwazi dhidi ya utamaduni wa usiri na porojo za kisiasa zinazoonekana kushamiri serikalini.

Zitto amesema kuendelea kuingiliwa kwa taasisi hizo kunasababisha mambo kufanyika ndivyo sivyo.

Ametoa mfano wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato akisema haieleweki mradi huo umeendeshwaje.

"Hatukatai Chato kuwa na uwanja wa ndege kwa sababu ni sehemu ya Tanzania; kinachoibua maswali ni namna mradi ulivyotekelezwa,” amesema.

Zitto amesema, "Hakukuwa na bajeti, zabuni hazikuwekwa wazi; aliyeshinda haijulikani ameshindaje na tunasikia hajawahi kujenga uwanja wowote."

Amesema taasisi za Serikali ikiwemo ofisi ya CAG na PPRA zilitakiwa zitoe taarifa ya kina kuhusu ujenzi huo.

Akizungumza katika mjadala huo, mwanzilishi wa mtandao wa JamiiForums, Maxence Mello amesema kuna haja ya Serikali kuongeza uwazi katika uendeshaji wa shughuli zake.

"Kuendelea kuweka mambo siri kunawafanya watu waibue vitu vingine ambavyo vingezuilika endapo wangekuwa wanafahamu kinachoendelea," amesema.

Mello amesema, "Kuficha mambo haisaidii na itasababisha Serikali iliyopo ikiondoka madarakani nyingine itakayochukua hatamu itaibua mambo ya ajabu."
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe Dogo na mwenzalo Mello.
    Mmekaa mkadiscuss mkafikia conclusion kuwa Serikali ya Awamu hii yetu ya Tano ,kuwa hamna Imani nayo na inafanya mambo yake kwa Siri kukuogopedni The Mighty Duo.
    Zubeli kabwe Zito Na huyu mwenzako mpya Mello.
    Hivyo ni Kweli? Je Mello ameshajiunga...!!! Nasikia Kadi za plastiki umechapisha nyingi
    Manake wahenga walinena Mshangaa ya Musa ya Firiuni yanamjia.
    Sasa Nimesikia Dira lako limeingia Masizi na kitambaa cha kufutia huna... Mie nnayo kilinexi
    je inaweza kusaidia.
    Zitto Zuberi Kabwe ... Kwa mara nyingine tena anawacha Uhusiano wa kimataifa na Itifaki kwa mahiga
    na kwenda anga za UENDESHAJI WA NCHI AKIWA KAMA MSHAURI MKUU WA JPJM NA MH K. MAJALIWA.

    NDUGU ZANGU DOGO HAJIELEWI WALA KUELEWA UTUMBO NA MADA ZISIZOLINGANA.

    SHAMRA SHAMRA ZA UAPISHWAJI VIPI ZILIENDA SHWARI.

    NIMESHAKUOMBEA KAZI KWA WATURUKI NA W/MAWASILIANO KATIKA UJENZI WA MADARAJA YA STD GAUGE RAIL.
    ZITTO ZUBERI KABWE USIILAZIE DAMU HIYO KAZI INAKUFAA NA TABIA ZAKO ZINALINGANA.
    MELLO ATAKUACHA KWENYE MATAA HIVI PUNDE. AKIONA WANACHAMA OLD TIMERS WAMEKUKIMBIA KWA TABIA YAKO.
    DOGO UNABOA ... TENA SANA.
    MIREMBE WANAKUSUBIRI FAILI KILA TUKIENDA LIKO MEZANI .. LINI UTARIPOTI .. NAKUONEA HURUMA DOGO

    SERIKALI YETU TUNA IMANI NAYO NA HAINA SIRI NA INA UTANDAWAZI KWA MAREFU NA MAPANA.. NYIE WAPINGA DILI ZA KIGAMBONI TSUNAMI IKO NJIANI... SI UNAELEWA.

    ReplyDelete
  2. zITO zUBERI kABWE ANASEMA....

    "jitihada hizo hazitakuwa endelevu endapo taasisi za uwajibikaji hazitaachwa zifanye kazi kwa uhuru na uwazi."

    sASA MIE NAMUULIZA zITO zUBERI kABWE.....??? Hayo Maneno umeyazungumzia Wapi huko twita au Fezi Buko??

    Naomba jibu lako. Na ulikuwa katika hali gani?
    Je hii mada uliandikiwa au Uliandika baada ya kufanya research?

    Huku nikingoja haya.... Mnnashindwa kuelewa wewe kama ulivyo na kiuhalisia wako.
    Unacho zungumza unakielewa au wanakubambikia Tu.

    Zitto Zuberi kabwe ... Unapatikana wapi na majira yepi?
    Hapa kuna walakini...lakini tutaujua ... Tafadhali tujuze.
    Wamebaki wangapi pale chamani ?? wenye mwelekeo kama wako!!??

    ReplyDelete
  3. Nnasikia Zitto Xuberi kambwe sasa hivi anajitayarisha katika Fani ya Bongo Fleva anatafuta wa kusapoti baada ya kuwachwa kwenye mataa chamani na wenye akili zao.
    Dogo anasikitisha amebaki peke yake na sasa ameamua kuigilia fani za kina Madee( R..si wa manzesee)

    ReplyDelete

Top Post Ad