Abiria Waonywa Kula Hovyo Wakiwa Safarini Msimu Huu wa Sikukuu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Abiria Waonywa Kula Hovyo Wakiwa Safarini Msimu Huu wa Sikukuu
Abiria wanaosafiri katika msimu huu wa kuelekea sikukuu wametahadharishwa kutokula au kunywa vitu watakavyopatiwa ndani ya magari na watu wasiowafahamu.

Pia wametakiwa kutoa taarifa kwa wakati pindi watakapoona kuna ukiukwaji wa sheria na kanuni za usafirishaji ikiwa ni pamoja na kutozwa nauli tofauti na iliyopangwa pamoja na mwendo kasi au mtu yeyote atakapofanya vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wao.

Rai hiyo imetolewa leo Ijumaa Desemba 15 wakati Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani Mtwara wakifanya operesheni katika mabasi ya abiria kituo kikuu cha Mtwara kabla ya kuanza safari ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa madereva, kondakta pamoja na abiria.

Akizungumza na abiria mkaguzi wa magari wa kikosi cha usalama barabarani, Said Masoud amewatahadharisha abiria kutokula hovyo vitu watakavyopatiwa kwenye magari na watu wasiowafahamu.

"Tunaelekea kipindi cha Krismasi na mwaka mpya ni kipindi cha hatari sana watu wako kazini, usimwamini uliyekaa naye kama humfahamu mmekutana kwenye kiti  anakupa pipi unakula, anakupa karanga unakula utaumia nawatahadharisha tena watu wapo kazini mmekutana kwenye gari salimianeni kama abiria ila usimuhisi kwamba hiyu ndio mwizi ili mkae kwa amani mfike salama," amesema Said.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad