Kala Jeremiah Amwahidi Zawadi Mama Samia Suluhu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kala Jeremiah Amwahidi Zawadi Mama Samia Suluhu
Baada ya msanii wa Hip Hop Kala Jelemiah kula shavu la nguvu la kusifiwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu kuwa ngoma yake mpya aliyoachia hivi karibuni “Kijana” amesema anajipanga kuilipa heshima hiyo aliyopewa na kiongozi wa nchini.

Akiongea kupitia eNEWZ ya     East Africa Television Kala amesema "nimefanya mziki kwa mda mrefu ila sijawahi kupata pongezi kutoka kwa kiongozi mkubwa wa nchi kama yule tena mbele za maelfu ya watu mara nyingi tumekuwa tukikutana na viongozi wa kawaida na kutupa pongezi za kawaida”.
Kala ameongeza kuwa alizipokea salamu za Makamu wa Rais kutoka kwa watu wengi  kitendo ambacho amekipokea  kwa mikono miwili na kuwa kauli hiyo ya Makamu wa Rais imempa deni la kuendelea kukaza buti na kuandaa nyimbo  nyingi  zitakazo kuwa mkombozi kwa Jamii.
Kala amemaliza kwa kusema  kauli ya Makamu wa Rais imempa faraja yeye na familia yake kwa ujumla na hata alipotumiwa kile kipande cha video ambayo Makam wa Rais alikuwa anamsifia aliiangalia mara nyingi kiasi kwamba hakuamini kitu ambacho alikuwa anakiona.
Msanii huyo wa Hip Hop kutoka Rock City anafunga mwaka kwa kauli yake ya kuwa hakuna mziki wa biashara bali kuna biashara ya muziki aliyoitoa hivi karibuni kupitia Enewz.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kala acha ujinga mdogo wangu sifa zinaua, unamaanisha utampa zawadi gani aliyo ikosa, au unataka kupigwa risasi na mumewe. Vijana kuna njia ya kusifia na kuna sifa rika kwa rika na siyo kila rika linastahili zawadi wengine tunastahili pongezi tuu.

    ReplyDelete

Top Post Ad