Diva Kuwaunganisha FA, Mr Paul na Heli Muziki

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Diva Kuwaunganisha FA, Mr Paul na Heli Muziki
Wasanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Mwana FA, Mr Paul na Heri Muziki ni moja ya wasanii wakongwe watakaosikika kwenye Album mpya ya ‘Ala za Roho’ ya Mtangazaji maarufu wa Radio Clouds FM, Diva The Bawse.

Hayo yamethibitishwa na Diva kwenye mahojiano yake na Bongo5, Ambapo amesema wakongwe hao amewakutanisha kwenye project yake mpya ambayo kwa sasa wapo studio kuipika na itakuwa moja ya ngoma kali zitakazokuwemo kwenye album yake.

“Nimefanikiwa kuwakutanisha Mwana FA, Mr Blue na Heri Muziki kwenye project mpya ambayo bila shaka itakuwa moja ya project kubwa zitakazopatikana kwenye album yangu ya ‘Ala za Roho itakayokuwa na nyimbo nane, ambayo itakuwa na wasanii wakongwe na wapya wa R’n’B A list kutoka Tanzania.“Amesema Diva.

Hata hivyo, Diva hajataja jina la ngoma ambayo amewashirikisha Mastaa hao watatu, Mwana FA, Heri Muziki na Mkongwe Mr Paul.

Akitaja baadhi ya majina ya Wasanii wa kisasa ambao watakuwemo kwenye album yake, Diva amesema watakuwepo Nandy, Heri Muziki na majina mengine makubwa.

Diva amesema album yake ya ‘Ala za Roho’ itatoka itatoka Februari 14, 2018 na itakuwa moja ya album bora za R’n’B kuwahi kutokea Tanzania.

“Ala za Roho itakuwa album ya kipekee kuwahikutokea Tanzania kwanza itakuwa na wasanii wengi wa A List ya Bongo Fleva, yaani hii itakuwa maana halisi ya Soul Music Album. Nawaahidi mashabiki wangu wakae mkao wa kula.“amesema Diva.

Akizungumzia uwepo wa wakongwe, Mwana FA na Mr. Paul, Diva amesema wote amewaweka kwenye ngoma moja ambayo tayari ameshairekodi na amesema itakuwa moja ya ngoma kali kutoka kwenye album yake.

“Unajua Mwana FA na Mr Paul ni watu ambao wanaheshima yao kwenye muziki wa Bongo Fleva, na mimi najiona mwenye bahati watu hawa kuwa kwenye album yangu, Ambayo tayari wamesharekodi na Heri Muziki na wimbo huo utakuwa kwenye album yangu ya ‘Ala za Roho’.“amesema Diva.

Akitoa sababu za kuachia album hiyo tarehe 14 Februari amesema mwezi Februari ni siku ya wapendanao na siku hiyo imebeba maudhui ya albumu yake.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad