Mradi wa Mwendo Kasi Waleta Heshima Dar Waleta Tuzo ya C40 Bloomberg

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mradi wa Mwendo Kasi Waleta Heshima Yaleta Tuzo ya C40 Bloomberg
JIJI  la Dar es Salaam ni miongoni mwa majiji 10 duniani ambayo yamepata tuzo ya C40 Bloomberg Philantropies 2017   kupitia Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka.

Katika tuzo hiyo  mwaka huu imepokelewa na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Miwta aliyerejea nchini alfajiri ya Desemba 8 mwaka huu.

Jiji la Dar es Salaam limechangia tuzo hiyo  na Jiji la New York  nchini Marekani

Mradi wa Mabasi yaendayo haraka unawahudumia abiria 200,000 kila siku kwa kutumia mabasi ya kisasa ambayo yanachangia kupunguza msongamano wa magari barabarani na kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa na hivyo kuwa siri ya mafanikio ya tuzo jijini hapa.

Tuzo ya C40 Bloomberg Philanthropies hutolewa kila mwaka katika miradi inayotekelezwa kwenye maeneo mahususi matano ili kutambua jitihada za majiji wanachama wa Taasisi ya mtandao wa Majiji zaidi ya 90 duniani inayoshughulika na namna bora ya kukabiliana na Athari za mabadiliko ya Tabia ya Nchi Duniani.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad