Polepole Awapiga Kijembe Vyama vya Upinza "Mwenyekiti Aseme Hela Ziko Wapi"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Polepole Awapiga Kijembe Vyama vya Upinza "Mwenyekiti Aseme Hela Ziko Wapi"
Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Humphrey Polepole amevipiga kijembe vyama vya upinzani akimtaka mwenyekiti wa moja ya vyama hivyo kusema hela ziko wapi.

Kupitia ukurasa wake wa “Twitter” Polepole amendika maneno hayo bila kufafanua ni mwenyekiti wa chama gani na hela za nini japo wafuasi wake wengi katika mtandao huo wamechangia mawazo wakitaja huenda ni hela za ruzuku.
Mbali na hilo Polepole pia amesema kuwa kile alichowahi kukitabiri kuwa upinzani hawataweza kushindana na chama chake siku za baadaye kimeanza kutimia.
Hii inatafsiriwa kama majibu kwa mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freman Mbowe ambaye hivi karibuni alitangaza chama chake hakitashiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge endapo Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) haitazifanyia kazi kasoro zilizojitokeza kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika mwezi Novemba mwaka huu.
“Nalipata kuwaambia wataweka mpira kwapani, wakasubiri siku kadhaa na hatimaye imekuwa. Kwa lugha ya shule ya msingi miaka ile ningesema "wameogopa kuputa", wangeputa waone namna ambavyo kwetu siasa za masuala zinalipa. Ushauri wangu: "Mwenyekiti" lazima aseme hela ziko wapi”, ameandika Polepole.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Lazima waweke 'mpira kwapani' sio kwa 'advatize' ile ya 42 kwa 1! Mugabe mjanja jamani, 'ka-skuti' akaona awashawishi 'manyumbu' wanaofuata mkumbo wajitoe, wakakubali kujitoa kwa sababu zisizo na kichwa wala miguu......nadhani siasa imewashinda, bora muanzishe bendi ya muziki iwe chadema jazz band kwakuwa MUGABE aliwahi kuwa DJ na anauzoefu wakutosha tu au kiwe kikundi cha singeli......INALIPA

    ReplyDelete

Top Post Ad