Rais wa Korea Kaskazini Apiga Marufuku Kuimba, Kunywa na Kufanya Mikusanyiko Wakati wa Kristmas

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais wa Korea Kaskazini Apiga Marufuku Kuimba, Kunywa na Kufanya Mikusanyiko Wakati wa Kristmas
RAIS Kim Jong Un wa Korea ya Kaskazini amepiga marufuku kuimba, kunywa vileo na kufanya mikusanyiko ya aina yote nchini humo wakati wa Krismasi mwaka huu.

Kwa mujibu wa shirika la ujasusi la Korea ya Kusini (NIS), hatua hiyo inakazia amri ya kupiga marufuku sherehe za Krismasi ya mwaka jana (2016) ikilenga kuzuia nguvu za upinzani nchini humo hususan sasa ambapo vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya nchi hiyo vinaonyesha kuiumiza nchi hiyo.


“Korea ya Kaskazini imeanzisha mfumo wa jumuia za chama tawala kuripoti matatizo ya kiuchumi ya watu wanayokumbana nayo kila siku, na imepiga marufuku mikusanyiko inayohusiana na unywaji wa vileo, uimbaji na burudani nyingine, na imeimarisha udhibiti wa habari kutoka nje,” lilisema NIS.

Fursa za kuitumia sikukuu hiyo kueneza uelewano na furaha zinazidi kufifia katika taifa hilo linalodaiwa kutawaliwa kidikteta na ambalo limepiga marufuku dini zote isipokuwa maadhimisho ya familia iliyoasisi taifa hilo la kikomunisti. Mwaka jana, Kim aliwazuia Wakristo nchini humo kuadhimisha Krismasi na badala yake akawataka kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa bibi yake, Kim Jong-suk, aliyezaliwa siku ya mkesha wa Krismasi mwaka 1919.

Akiwa Mkomunisti aiyebobea, mke wa kwanza wa mwasisi wa taifa hilo la kikomunisti, Kim Il Sung, anafahamika kwa wananchi wa Korea ya Kaskazini kama “Mama Mtukufu wa Mapinduzi”. Miti yenye mapambo ya kuadhimisha Krismasi huonekana katika maduka makubwa ya bidhaa jijini Pyongyang, lakini hakuna alama zozote za kidini.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni propaganda za Korea kusimi kwa ndugu zao wa damu. Korea kusini ni kitumushi fulani au kibaraka wa mataifa fulani ya magharibi yenye nguvu yanayofanya kila njia kuhakikisha North Korea haiwi China ya pili kimaendeleo. Mataifa ya Magharibi wanahofia sana kuwa na taifa jengine la kikomunisti lenye nguvu duniani. Wataalamu wa mambo watakwambia kuwa wakorea kaskazini kama wataachiwa kufanya mambo yao wanavyotaka basi hakuna taifa lolote duniani lingewakaribia kimaendeleo si Marekani si China huo ndio ukweli. Kuhakikisha kuwa wanadhibitiwa basi wamemuundia ndugu yake kuwa ndie adui yake namba moja. Na Korea kusini inapata karibu kila kitu inachokihitaji kutoka kwa wanaomlea kuhakikisha wanamdhibiti North Korea hii Dunia ina mambo sana we acha tu.��

    ReplyDelete

Top Post Ad