Tunda Man Awachana Wasanii Wanaotoa Nyimbo Kila Kukicha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Tunda Man Awachana Wasanii Wanaotoa Nyimbo Kila Kukicha
Kapteni wa Bongo Fleva Tundaman amewataka wasanii waache tabia ya kutoa toa nyimbo kila kukicha wakati nyimbo zenyewe mbovu na hazidumu kwa muda mrefu.

Akiongea na eNEWZ ya East Africa Television, Tunda Man amesema nyimbo zake anazoziandika zinaishi kwa mda mrefu na zinamaudhui yanayojitosheleza kuishi miaka mingi katika sanaa na ndio maana amekaa zaidi ya miaka miwili  tangu ameachia nyimbo yake ya mwisho Mama Kijacho.
Hata hivyo Tundaman anasema pamoja na wasanii wa sasa kuachia nyimbo nyingi kwa wakati mmoja, lakini wengine wanaachia nyimbo ambazo hazina ujumbe wala maana kwa jamii. “Wanatoa nyimbo mbaya ambazo zikipigwa kwenye vyombo vya habari wiki mbili tatu tu mwisho wa siku zinapotea kabisa”.

Tundaman pia ameongelea suala la wasanii kubebwa ambapo amesema katika mziki wa sasa wasanii wamekuwa wanabebwa mara nyingi kwenye vituo mbalimbali vya Radio na Television. Mklai huyo wa 'Hit' kibao ameachia ngoma yake mpya inayoitwa TOTO.
“Wakati mwingine unakuta mtu anatoa nyimbo ambayo hajaigharamia kwa chochote kwa kuwa tayari ana washikaji wengi watakao msaidia katika Video na hata Audio mwisho wa siku inatoka nyimbo mbaya au ambayo haina viwango” amesema Tundaman.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad