Malaria yamtesa Tambwe Arudishwa Dar

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Malaria  yamtesa Tambwe Arudishwa Dar
Wakati klabu ya Yanga leo ikitarajia kuingia dimbani kucheza na Singida United kwenye michuano ya Mapinduzi, imemrejesha Dar es salaam mshambuliaji wake Amissi Tambwe kwasababu ya kuugua.


Mshambuliaji huyo raia wa Burundi mchana huu amelazimika kuondoka kambini mjini Zanzibar kurejea Dar es Salaam mchana huu kwaajili ya matibabu zaidi kufuatia kusumbuliwa na homa.

Daktari wa timu hiyo Edward Bavu amesema kuwa Tambwe amekuwa akisumbuliwa na Malaria kwa takribani siku nne. "Ana malaria, kwa siku zaidi ya nne sasa amekuwa na wakati mgumu, tumelazimika kumrejesha Dar es salaam ili apate matibabu zaidi'', amesema Dr. Bavu.

Mrundi huyo amekuwa katika msimu mgumu, akianza kukaa nje tangu Agosti 2017, kutokana na maumivu ya goti kabla ya kurejea mwezi Desemba, lakini mapema leo ameoondolewa tena kambini kwa sababu ya Malaria.

Kuugua kwa Tambwe kunazidi kuipunguzia nguvu safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo ambayo pia inawakosa nyota wake Mzimbabwe Donald Ngoma na Mzambia, Obrey Chirwa.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad